Migogoro
Zaidi ya watu 7,000 wauawa kutokana na machafuko Kongo
24 Februari 2025Matangazo
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Judith Suminwa Tuluka amesema karibu watu 7,0000 wameuawa tangu mwezi Januari katika mapigano mashariki mwa nchi hiyo.Congo yataka ukiukwaji wa haki uchunguzwe Goma
Suminwa ameliarifu hayo Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva mapema hii leo. Amesema karibu watu 450,000 hawana makazi na hasa baada makambi ya wakimbizi wa ndani kuharibiwa.
Hatua ya waasi wa M23 ya kuchukua maeneo, inachukuliwa kama mzozo mbaya kabisa katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja wa mzozo huo.