Asili na mazingiraUturuki
Watu 50,000 wahamishwa Uturuki kuepuka moto ya nyika
30 Juni 2025Matangazo
Vikosi vya zima moto vinapambana na msururu wa mioto hiyo ya nyika huku moto mkubwa zaidi ukiripotiwa katika mkoa wa Izmir magharibi mwa Uturuki. Shirika la kitaifa la kudhibiti majanga AFAD limesema raia 50,000 waliohamishwa ni kutoka vitongoji 41.
Hayo yanaripotiwa wakati mataifa kadhaa ya Ulaya ikiwa ni pamoja na Uhispania, Ureno, Italia na Ufaransa yakiripoti wimbi la joto kali, huku yakitoa tahadhari za kiafya na uwezekano wa kutokea kwa mioto ya nyika.
Siku ya Jumapili, Ureno ilivunja rekodi ya viwango vya juu vya joto kwa kufikia nyuzi 46.6 kipimo cha Celcius katika wilaya ya Mora jimboni Alentejo.