JangaAfrika
Hatma ya watu 40 haijulikani baada ya boti kuzama Nigeria
18 Agosti 2025Matangazo
Chombo hicho kilichopata ajali kilikuwa kimewabeba watu wasiopungua 50 waliokuwa wakielekea kwenye soko maarufu la Goronyo katika jimbo la Sokoto. Mkuu wa huduma za dharura Zubaida Umar amesema, idara yake inashirikiana na mamlaka nyingine za ndani kuwatafuta na kuwaokoa watu ambao bado hawajapatikana.
Wiki tatu zilizopita watu 13 walikufa maji na makumi wengine walitoweka baada ya boti nyingine kuzama ikiwa na abiria wasiopungua 100 katika jimbo la Niger la nchini humo.