Watu 30 wameripotiwa kuuawa na RSF nchini Sudan
17 Agosti 2025Matangazo
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Mtandao wa Madaktari wa Sudan. Taarifa ya mtandao huo iliongeza kwa kusema shambulio hilo lililenga kambi ya Abu Shouk pembezoni mwa mji wa El-Fasher, ambapo majeruhi walitibiwa katika mazingira magumu sana ya kibinadamu na kiafya.Mji huo umekumbwa na uhaba mkubwa wa dawa, wahudumu wa afya, na chakula kutokana na mzingiro wa RSF.Umoja wa Mataifa unasema kambi ya Abu Shouk imeshambuliwa na kundi la RSF kwa mara 16 kati ya Januari na Juni, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200 na kujeruhiwa kwa zaidi ya 100.