MigogoroAfrika
Watu zaidi ya 100 wameuwawa kwenye shambulio Sudan
13 Aprili 2025Matangazo
Ripoti za awali kutoka shirika moja la misaada ya kibinadamu zimeeleza kwamba watu 57 waliuawa siku ya Ijumaa, wakiwemo raia 32 waliouawa El-Fasher na 25 waliouawa katika kambi ya Zamzam.
Jeshi la Sudan lilithibitisha vifo hivyo na kuongeza kwamba katika shambulio hilo raia 74 waliuwawa huku wengine 17 wakijeruhiwa.
Shirika la Sudan la Kulinda Raia limesema waliouawa ni pamoja na wafanyakazi tisa wa misaada ya kibinadamu waliokuwa wakifanya kazi katika hospitali ya Zamzam inayosimamiwa na shirika lisilo la kiserikali la kimataifa.
Soma pia:Watu 25 wauwawa katika kambi ya wakimbizi Sudan
Hakukuwa na tamko lolote la kuhusika na shambulio hilo kutoka kwa kundi la RSF. Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio hilo baya dhidi ya raia.