MigogoroAfrika
Zaidi ya wapiganaji 40 wa Al shabaab wauawa Somalia
2 Machi 2025Matangazo
Televisheni ya taifa nchini Somalia imesema kupitia mtandao wa kijamii wa X kwamba zaidi ya wanachama 40 wa kundi wa wapiganaji wa Al Shabaab wameuawa katika operesheni ya jeshi la taifa nchini humo kwa ushirikiano na washirika wa kimataifa katika eneo la Biya Cadde lililopo katika jimbo la Hirshabelle leo Jumapili.
Soma pia: Shambulio la Marekani lamlenga mpanga mikakati wa IS Somalia
Televisheni hiyo ya taifa imeongeza kwamba bado jeshi la Somalia, washirika wake wa kimataifa na wenyeji wanaendelea na operesheni hiyo.
Somalia imekuwa ikiratibu operesheni mbalimbali za kuwadhibiti wanamgambo wa Al Shabaab ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi mara kwa mara nchini Somalia.