Zaidi ya Waislamu milioni moja wawasili Mekkah
2 Juni 2025Matangazo
Zaidi ya Waislamu milioni moja wamemiminika katika mji mtakatifu wa Mekka nchini Saudi Arabia kwaajili ya kushiriki ibada ya mwaka huu ya Hijjah.
Mamlaka nchini humo zimeahidi kuhakikisha ibada hiyo inafanyika kwa njia salama kutokana na ongezeko kubwa la joto. Kadhalika mamlaka za Saudi Arabia zimekuwa zikiendesha operesheni kubwa ya kudhibiti wageni walioingia kinyume cha sheria.
Ibada ya Hajjambayo ni moja kati ya nguzo tano zinazoujenga Uislamu hufanyika kila mwaka ambapo mwaka huu inatarajiwa kuanza rasmi siku ya Jumatano wiki hii.
Ripoti kutoka mamlaka za Saudi Arabia zimesema,kufikia siku ya Ijumaa zaidi ya mahujaji milioni 1.3 walikuwa wameshawasili nchini humo kwaajili ya kushiriki ibada hiyo.