Zaidi ya waandamanaji 340 wakamatwa Uturuki
22 Machi 2025Mamlaka nchini Uturuki imesema zaidi ya watu 340 wamekamatwa kufuatia maandamano makubwa zaidi ya barabarani nchini humo yaliyochochewa na kushikiliwa kwa meya wa mji wa Istanbul, Ekrem Imamoglu.
Mamia ya maelfu ya watu wameingia barabarani nchini kote na kusababisha makabiliano na polisi wa kutuliza ghasia katika miji mitatu mikubwa nchini Uturuki ya Istanbul, mji mkuu Ankara na mji wa pwani wa magharibi wa Izmir.
Soma zaidi: Wajumbe wa amani wa Urusi na Ukraine kukutana Saudia
Kwa siku tatu mfululizo waandamanaji wanaandamana kumuunga mkono Imamoglu ambaye ni mpinzani mkubwa wa kisiasa wa Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye kukamatwa kwake Jumatano kumezusha sintofahamu kote nchini humo.
Kiongozi huyo anatarajiwa kupandishwa kizimbani tena leo kwa mara ya pili kujibu tuhuma zinazomkabili za ugaidi ambazo hata hivyo amezikanusha.