Hali yasalia kuwa tete mjini Istanbul kufuatia maandamano
24 Machi 2025Mamlaka nchini Uturuki imesema, inawashikilia zaidi ya watu 1,100 kufuatia maandamano makubwa yaliyozuka wiki iliyopita baada ya kukamatwa meya wa mji wa Istanbul na mpinzani mkuu wa rais wa nchi hiyo Recep Tayip Erdogan, Ekram Imamglo.
Maandamano hayo ya maelfu ya watu yalianza mjini Istanbul baada ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa upinzani na kuenea katika zaidi ya majimbo 55 kati ya 81 ya Uturuki, na kusababisha makabiliano na polisi wa kutuliza ghasia na kulaaniwa kimataifa.
Mbali na kukamatwa kwa watu hao, Uturuki imekuwa ikizifungia akaunti mbalimbali za mitandao ya kijamii za watu wanaohamaisha maandamnao nchini humo.Mahakama ya Uturuki yaamuru kuzuiliwa kwa Meya wa Istanbul
Hali kadhalika, Ekram Imamglo anayetuhumiwa kwa ufisadi na ugaidi anatajwa kuwa mwanasiasa pekee ambaye anaweza kumshinda rais wa Uturuki Erdogan katika uchaguzi mkuu ujao na tayari chama chake cha CHP kimempitisha kwa mgombea mkuu katika uchaguzi wa 2028.