Raia wapya nusu milioni wa Ujerumani kupiga kura mwaka huu
21 Februari 2025Matangazo
Kulingana na Ofisi ya Takwimu ya Ujerumani, tangu uchaguzi uliopita wa mwaka 2021, idadi ya watu waliopata uraia nchini humo imeongezeka kwa kasi. Zaidi ya watu 500,000 walipata uraia wa Ujerumani kati ya mwaka 2021 na 2023.
Wengi wa raia hao wapya ambao watapiga kura siku hiyo ya Jumapili, wameelezea mchanganyiko wa hisia na matumaini ya mabadiliko, pamoja na uhamasisho kuhusu haki zao za kupiga kura .
Friedrich Merz, kiongozi wa upinzani anaetaka kumrithi Scholz
Baadhi yao wana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa umaarufu wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD kinachopinga uhamiaji.