MigogoroAfrika
Zaidi ya askari 1,300 wa Kongo wahamishwa kutoka Goma
16 Mei 2025Matangazo
Taarifa ya shirika hilo imesema hadi kufikia jana Alhamisi, watumishi 1,359 wa vyombo vya dola waliokuwa wameomba hifadhi kwenye kambi za ujumbe wa kimataifa wa kulinda amani nchini Congo, MONUSCO, wamehamishwa pamoja na familia zao na kupelekwa mji mkuu Kinshasa.
Shirika hilo limeeleza kuwa operesheni hiyo ilikuwa "ngumu" na ilihusisha mashauriano marefu kati yake, serikali, ujumbe wa MONUSCO pamoja na kundi la M23.
Inaarifiwa kundi hilo lilikataa zoezi hilo kufanyika kupitia uwanja wa ndege wa Goma ambao wameufunga tangu walipoukamata mji huo mapema mwaka huu.