MigogoroIsrael
Zaidi ya Wapalestina 50,000 wameuwa katika vita vya Gaza
23 Machi 2025Matangazo
Takwimu hizo ambazo hazitofautishi kati ya wapiganaji na raia, haijathibitishwa na baadhi ya duru za kujitegemea, lakini mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa yamesema takwimu hizo zinaaminika kwa kiasi kikubwa.
Kulingana na ripoti ya vyombo vya habari , jumapili (23.03.2025) karibu watu 30 waliuawa katika mashambulizi mapya ya Israel kusini mwa Gaza.
Shirika la habari la Palestina WAFA, limeripoti juu ya mashambulizi mbalimbali, yakiwemo mashambulizi ya droni, katika maeneo ya Rafah na Khan Younis.
Awali, jeshi la Israel lilitoa onyo kwa wakazi wa Tal al-Sultan wilaya moja wapo katika eneo la Rafah kwamba "litaanzisha mashambulizi kuyalenga mashirika ya kigaidi", na hivyo kuwalazimisha wakazi kuondoka kutoka kwenye maeneo hayo.