Klabu ya Yanga SC ya Tanzania imefagia mataji yote msimu huu baada ya kubeba Kombe la Shirikisho kufuatia ushindi wa 2 – 0 dhidi ya Singida Black Stars mechi iliyochezwa visiwani Zanzibar. Nchini Kenya miamba ya kandanda na mabingwa wa kihistoria nchini humo Gor Mahia waoneshwa kivumbi baada ya kupata kichapo cha 2-1 na mabingwa wa ligi ya Daraja la pili Nairobi United waliobeba Kombe la FKF.