Yanga Princess wapania ushindi Dabi ya Kariakoo
17 Machi 2025Yanga Princess wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa Machi 2 Mfululizo na Simba wakifungwa 1 bila na mechi ya mkondo wa kwanza wakifungwa goli 3 -1 katika msimu wa 2023/24.
Mapema leo Kocha wa Yanga katika mkutano na Waandishi wa Habari "Tumeendelea kufanya mazoezi tukiamini ni Mchezo muhimu kwa sababu Simba ni Timu nzuri na wanaongoza Ligi na Mchezo wa kesho utakuwa mgumu na mzuri kutokana na matokeo ambayo tunayoyapata kila tupokutana na Simba "Alisema Kocha wa Yanga Edina Lema.
"Mechi ya kesho ni Muhimu sana kwetu tupo Tayari na hatutaki kuwaangusha mashabiki wetu Alisema kocha wa Simba Yassifu Basigi"
"Miongoni mwa malengo tuliyojiwekea ni pamoja na kushinda mechi ya kesho ya watani wa Jadi alisema Nahodha wa Simba Violeth Nicholaus
Ugumu wa mechi pia upo katika mbio za ubingwa katika Msimamo wa ligi kuu ya wanawake Ili simba aendelee kujichimbia kileleni anahitaji ushindi wa Dabi ya kesho pamoja na kwamba Simba Queens yupo kileleni na alama 34 lakini anayemfukuzia nafasi ya 2 ni Jkt Queens alama 32 lakini ukiangalia Yanga Yanga watofautiana alama 10 na simba wakiwa na alama 24.
Ligi ya mabingwa Ulaya
Mbali na mechi hii mashabiki wa kandanda la wanawake vile vile wanasubiri kwa hamu mechi za robo fainali Ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo Real Madrid na Arsenal.
Mechi ya marudiano inatarajiwa Machi 26,2025 ili kupata mshindi atakayefuzu hatua ya nusu fainali ya Ligi hiyo maarufu ulimwenguni.
Wapinzani wa ndani Chelsea na Manchester City wanakutana mjini Manchester katika mechi yao ya kwanza.
Tanzania Taifa Stars
Na Maandalizi ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Chini ya Kocha Hemed Morocco Yameanza Rasmi kwani Tayari kikosi kimeingia kambini kujiwinda na Mchezo wa Kufuzu Kombe la Dunia 2026 ambapo watakuwa na kibarua kigumu Mbele ya Morocco March 26.