Yaliyochambuliwa na wahariri wa Ujerumani hii leo
30 Agosti 2005
Kuhusu tufani “Katrina” gazeti la SÜDWEST-PRESSE la mjini Ulm limeandika:
“Dharuba iliyopiga karibu na mwambao wa Louisiana ilikua faraja kwa masoko ya mafuta.Hoja nyengine wameipata kupandisha bei ya mafuta.Japo kama visima vilivyosimamishwa kwasababu ya kuhofia kimbunga “Katrina”si vingi kuweza kuhalalisha uamuzi wa kupandisha bei ya mafuta kwa dala tatu kwa pipa.”
Kinyume na SÜDWEST-PRESSE,gazeti la TAZ la mjini Berlin linatanguliza mbele hifadhi ya hali ya hewa,na linaandika:
“Picha za vijiji vilivyofura,matope yanayotiririka,magunia ya michanga kila pembe,-ndio kwanza picha hizo za mafuriko ya msimu wa kiangazi barani Ulaya zimeanza kuondoshwa katika televisheni. Unaweza kusema picha za maafa mtindo mmoja.Wataalam lakini wanaonya,kuanzia sasa,picha kama hizo tutakua tukiziona kila wakati.Kimsingi kile walichokiashiria miaka kadhaa iliyopita ndio kwanza sasa kinachomoza.Mabadiliko ya hali ya hewa yasiyoepukika yaliyosababishwa na binaadam .Hakuna ishara kwamba hali hii itabadilika.Wanaviwanda wanahoji eti hifadhi ya hali ya hewa itagharimu ukuaji wa kiuchumi.Ndo kusema hakuna lolote la kufanya?Bila shaka lipo.Picha zinabidi zitupe moyo na kufuata nasaha ya wataalam linapohusika suala la kuhifadhi hali ya hewa.”
Hata gazeti la mjini Cologne,Kölner Stadt Anzeiger linaamini kimbunga Katrina ni onyo la kuchafuliwa hali ya hewa.Gazeti linaandika:
“Mjini Washington,usemi wangali nao bado wabishi wasiotaka kuutambua uwiano kati ya moshi unaotoka viwandani,moshi unaoenezwa na binaadam hewani na kuzidi kupanda hali ujoto ulimwenguni.Lakini shaka shaka,ambazo zinastahiki,wanasiasa wanaziangalia kua ni pingamizi.Maafa ya papo kwa papo yaliyosababishwa na hali ya hewa miaka ya hivi karibuni-yote yanaashiria kimoja—ikimaanisha-“fuateni uzi huo huo” .Bila ya marekebisho katika sera za hifadhi ya hali ya hewa nchini Marekani ,basi hata ulaya wale wanaopaza sauti na kuhoji eti hifadhi ya hali hewa, kwa mtazamo wa muda mfupi,inaambatana na gharama,hawatanyamaza.”
Mada ya pili iliyochambuliwa na wahariri wa magazeti hii leo jumanne inahusu azma ya mtetezi wa kiti cha kansela Angela Merkel,ya kuiteuwa tume ya wataalam wa kiuchumi itakayoongozwa na Heinrich von Pierer.
Gazeti la Handelsblatt la mjini Düsseldorf linaandika:
“Heinrich von Pierer,kiongozi wa zamani wa kampuni la Siemens,anatakiwa aongoze tume ya watu kumi wenye ujuzi wa hali ya juu wa kiuchumi ili kumshauri Angela Merkel vipi kuchochea ukuaji wa kiuchumi na mwamko katika jamii.Kamisheni za wataalam ni jambo la maana:Mtu anaweza kuunda kamisheni hizo kwa kuwajumuisha watu kadhaa mashuhuri na sherehe za kila aina kufanyika na upatu kupigwa, kamisheni hizo zinapozinduliwa.Ripoti za kila aina zinaweza kuandikwa na kubainisha,watu hawajapakata mikono,mageuzi yanayofikiriwa kutiwa njiani yanazingatiwa kwa makini.Lakini kisiasa hakuna lolote la lazima.”
Gazeti la NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG linalalamika,kuteuliwa Heinrich von Pierer kama mshauri tuu,haitoshi.Gazeti linaandika:
“Kuna kasoro hapa,kwamba von Pierer ateuliwe kua mshauri mkuu tuu bila ya matumaini ya kua waziri-si jambo linaloingia akilini.Kwasababu bila ya kua na wadhifa serikalini,ushauri wake hautakua na uzito wowote katika maamuzi ya kisiasa ,seuze tena kamisheni za wataalam zipo tena za kila aina.Serikali mara nyingi inaunda kamisheni kama hizo kwa kisingizio tuu ili baadae ikwepe kupitisha maamuzi yasiyovutia.”
Gazeti la LÜBECKER NACHRICHTEN linahisi kwa vyovyote vile uamuzi wa Angela Merkel ni wa maana.Gazeti linaandika:
“”Mamoja,jukumu atakalokua nalo Heinrich von Pierer katika kundi la Angela Merkel litakua la aina gani.Kua na mtu kama huyo katika kampeni ya uchaguzi ni ufanisi.Siemens ni jina maarufu la viwanda nchini Ujerumani.Mkuu huyo wa zamani wa kampuni hilo mashuhuri ulimwenguni,ni shahidi kwamba Merkel pia anaweza kusikilizana na mabosi wa kiuchumi.Sifa hii hadi sasa alikua akijivunia Gerhard Schröder tuu,na Angela Merkel akionekana mgeni katika uwanja huo.Pengo katika uwanja wa kiuchumi na fedha,lililoachwa na Friedrich Merz-limezibwa kwa sehemu na Kirchhof.Na jina la von Pierer bila shaka linaleta nuru katika sera za kiuchumi za Angela Merkel.