Yaliyoandikwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani
4 Julai 2006Maridhiano ya vyama vinavyounda serikali kuu ya muungano mjini Berlin,CDU/CSU na SPD kuhusu mageuzi ya mfumo wa bima ya afya ndio yaliyotangulizwa mbele hii leo na wahariri wa magazeti ya Ujerumani.
Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linayakosoa maridhiano hayo na kuandika:
„“Muungano wa vyama vikuu umeahidi makubwa ,walichokitoa lakini ni punje.Vyama ndugu vya CDU na CSU pamoja na chama cha SPD vilidhamiria kuufanyia mageuzi ya kina mfumo wa bima ya afya,lakini hakuna cha maana kilichobadilishwa.Ilikua michango katika bima ya afya ipunguzwe na kodi za mapato zipandishwe-sasa lakini yote hayo yamepanda.Wanataka kulazimisha mashindano kati ya mashirika ya bima ya afya yanayomilikuwa na serikali-sasa lakini imebainika upande mmoja kati ya vyama hivyo,unapigania masilahi ya mashirika ya umma na upande wa pili unapigania yale ya mashirika ya kibinafsi.Hiyo sio ladha ya siasa kansela Angela Merkel aliyoiahidi-ni shira inayonata,na ladha yake haitofautiani hata kidogo na aile ya enzi za Helmut Kohl na Gerhard Schröder-linahisi gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG.
Hata gazeti la mjini Cologne,KÖLNISCHE RUNDSCHAU linahisi hakuna chochote cha maana kilichofikiwa.Gazeti linaandika:
„Tutabakia pale pale na kuendelea na tabia yetu kutaka kila kitu kidhaminiwe kikamilifu na bima ya afya-tutaendelea kuwa washika usukani wa wameza vidonge wakubwa ulimwenguni –licha ya bei za vidonge hivyo kua juu kupita kwengineko kokote kule duniani.Hakuna kitakachobadilika pia ,madaktari wataendelea kuzongwa zaidi na makaratasi na kazi za kuratibu badala ya kuwashughulikia wagonjwa.Na wala hakuna dalili kwamba mashirika ya bima ya afya yatajikuta siku moja yakilazimika kupunguza shuighuli zake.Kiwango cha chini cha uzazi na gharama zinazozidi kukua za huduma za afya,yote hayo yatachangia kuifanya sera ya afya iendelee kwa muda mrefu kua mada ya mivutano humu nchini „linaashiria gazeti la KÖLNISCHE RUNDSCHAU.
Mhariri wa gazeti la DIE RHEINPFALZ la mjini LUDWIGSHAFEN amekasiri,zaidi,miongoni mwa mengineyo na nyongeza ya asili mia sifuri nukta tano ya malipo ya bima ya afya.
„Kichekecho kikubwa hichi,hasa kwakua nyongeza hii inakuja katika wakati ambapo tayari kodi ziada imepandishzwa kuanzia mwaka 2007-na kodi hiyo inahusu pia madawa.Na kwakua baadhi ya mashirika ya bima yasiyokua na fedha za kutosha bado hayatosheki,si hasha malipo ya bima yatapanda tena.Raia analazimika kulipa mara dufu na penegine hata mara tatu kwasababu ya woga na ukosefu wa fikra kutoka kwa wanasiasa“ linasisitiza gazeti la Die RHEINPFALZ.
Gazeti la WESTDEUTSCHE ZEITUNG la mjini Düsseldorf linahisi
„Vile vielelezo vya marekebisho ya mfumo wa bima ya afya,vinamvunja mtu moyo kwa namna ambayo mtu angependelea kuiomba serikali kuu ifunge virago na kuwafuata waargentina na wa-Brazil.Mpango unaotajikana kua muhimu kupita yote ya serikali hii ya muungano wa vyama vikuu,umesukumwa kwa mguu wa shoto uwanjani,kwa namna ambayo hakuna anaecheka.Kwa jumla mtu anaweza kusema,hakuna kilichobadilika-michango ya bima ya afya tuu itapanda-na hata hayo si mepya.
Gazeti la OSTSEE ZEITUNG la mjini Rostock linakosoa:
„Lengo halisi lililokuwepo,yaani kupunguza gharama za soko la ajira,ili kuweza kubuni nafasi zaidi za kazi,limeachwa kando.Badala ya kupunguza matumizi na kuleta mageuzi ya kina katika mfumo mzima wa afya,serikali ya muungano wa rangi Nyeusi na Nekundu imekubaliana na kile inachokiweza zaidi-yaani siasa ya mkono mrefu.