Yaliyoandikwa magazetini nchini Ujerumani hii leo
16 Novemba 2005
Platzeck amejipatia takriban kura za wajumbe wote waliohudhuria mkutano mkuu wa SPD.Gazeti la Kölnische Rundschau linaandika:
“Ni matokeo ya kusisimua naya ajabu pia kwa kiongozi mpya wa SPD Matthias Plaatzeck –hakuna tena kuwatia adabu wakorofi kama vile Andrea Nahles au Bärbel Dieckmann.Wana SPD wanajivunia masikilino na mshikamamo ambao si wakawida.Kwani ajabu?Hasha.Baada ya mitafaruku na vuta vikuvute ya wiki zilizopita,isingukua muwafak kwao kuendelea kuzozana kwa sasa.Uongozi mpana wa chama cha Social Democratic ulisababisha kujiuzulu mwenyekiti anaeheshimiwa sana chamani.Hali hiyo imewaudhi wengi chamani na kuwafadhaisha pia madhamana .Mchezo wa kupigania madaraka unaonyesha umemalizika,angalao kwa muda kuanzia sasa.”
Hata gazeti la MANNHEIMER MORGEN linaleta uwiano kati ya SPD na kiongozi wake mpya.Gazeti linaandika:
“Kwa kumchagua Platzeck kua mwenyekiti wake,Wasocial Democratic wamedhamiria sio tuu kujihakikishia matokeo bora ya uchaguzi katika majimbo mepya ya Ujerumani,bali pia kua na aina mpya ya uongozi katika nyakati tulivu na za kutia moyo.Na hotuba yake imepindukia matarajio.Mwanasiasa huyo wa kutoka Postdam amewanyooshea mikono wana SPD wote,amewapa moyo na kuwatanabahisha wayachukuliwe mageuzi kua ni fursa ya maendeleo.Platzeck ameibuka na ushindi na kunawiri katika uongozi wa chama cha SPD,ila Hubertus Heil tuu,ndie aliyepwaya alipochaguliwa kua katibu mkuu.Wana SPD wanaondoka Karlsruhe wakiwa na imani hali mpya iliyochomoza itadumu.Na kila mmoja anawaombea heri kwasababu nchi hii inahitaji watu wenye matumaini mema na kuona mbali.
Gazeti la HEILBRONNER STIMME nalo pia linaamini SPD itanawiri baada ya mkutano mkuu wa Karlsruhe.Gazeti linaandika:
“Njia gani itafuatwa na SPD chini ya uongozi mpya?Chama hicho kinakabiliwa na changamoto kubwa;Franz Münterfering akiwa miongoni mwa wenye usemi katika siasa za serikali kuu na Matthias Platzeck akipewa jukumu la kusimamia hatima ya chama hicho.Kuelezea malengo peke yake,haitoshi.Katika kipindi cha miaka miwili ijayo SPD inabidi iwe imeshabuni muongozo jumla wa kufuatwa.Itakua fursa hapo ya kufufua upya utaratibu wa kujadiliana.Na itakua fursa pia kwa Platzeck kukielekeza chama cha SPD vkama anavyokusudia.-
Gazeti la NEUE RUHR ZEITUNG la mjini Essen linatia shaka shaka kidogo:Gazeti linaandika:
“Kuungwa mkono kwa asili mia 99.4,akiongoze chama cha SPD,ni ushahidi timamu unaoashiria kile kinachomsubiri kiongozi huyo mpya.Ni wachache tuu wanaojua kile anachokiweza.Hotuba ya kusisimua aliyoitoa baada ya kuchaguliwa mjini Karlsruhe,haimaanishi kama kila kitu atakiweza.Ni ahadi tuu.Kuna wale ambao wanajifunza wanapojikuta mbele ya mitihani.Ama kwa upande wa Platzeck kuna wanaompa muda hadi fungate pamoja na SPD itakapomalizika,mivutano ya mwanzo kuchomoza na wapinzani wa kweli kujitokeza.Kiongozi mpya analazimika kuweka wezani sawa kati ya shughuli za serikali na kitambulisho cha chama chake.
Gazeti la mjini Bonn General Anzeiger linahisi haitakua kazi rahisi:Gazeti linaandika:
“Matokeo ya karibu mia bin mia hayatobadilisha chochote .Yanaonyesha tuu kwamba wajumbe wanapendelea kuyaacha kando mashaka yote ya wiki zilizopita.Lakini ishara za mshikamano alizozitoa jana Matthias Platzeck na kushangiriwa na wajumbe mkutanoni-zimegubikwa na hali ya kutojua nini cha kufanya katika chama hichi cha SPD,ambacho,na hapa isisahauliwe,kinajikuta katika hali ya kumomonyoka vibaya sana tangu upande wa wanaachama wake mpaka kufikia wabunge wake-hali ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu mwaka 1953.
Gazeti la THÜRINGER Allgemeine la mjini Erfurt linahisi matokeo hayo yanaashiria mapambano ya kuania madaraka.gazeti linaandika:
“Du asili mia 99.4 ya kura!Hata Honecker yangemchoma.Hasa kwa kua uchaguzi huo ulikua wa siri.Kiongozi huyo mpya anajivunia sifa kubwa alizojipatia wakati wa mafuriko katika sehemu ya mashariki ya ujerumani alipokua waziri wa mazingira katika serikali ya Brandenburg.Sifa kama hizo zinatia moyo.Lakini kama sifa hizo zinatosha kweli kuongoza chama sawa na alivyovalia viatu vya mvua kusimamia shughuli za uokozi-ni suala jengine.Hana maarifa yoyote ya uongozi tuseme katika tawi la vijana wa SPD,hajawahi kujishughulisha na shughuli za chama hicho,hadi wakati huu Platzeck mtu anaweza kusema amekua pembezoni mwa chama na sio kileleni.Na zaidi ya hayo hana uzowefu wa kukabiliana na mitihani ya kuania madaraka ambayo kawaida haiishi chamani.