Yaliyoandikwa magazetini nchini Ujerumani hii leo
15 Desemba 2004Kuhusiana na mada ya nakisi ya bajeti iliyopindukia masharti ya umoja wa Ulaya ya kudhamini utulivu wa sarafu ya pamoja Euro,gazeti la mjini Gera,OSTTHÜRINGER ZEITUNG linajiuliza:Imekwenda kwendaje kamisheni kuu ya umoja wa Ulaya ikabadilisha hukmu yake kuelekea bajeti ya serikali kuu ya mjini Berlin.Ndo kusema uhusiano kati ya serikali ya shirikisho na kamisheni kuu haujaingia dowa kutokana na mvutano usiokwisha kuhusu bajeti ya Ujerumani?Baraka hii ya kabla ya krismasi pengine ina sababu zake:Tarakimu za Ujerumani hazikuboreka,kwa hivyo hoja za kamisheni kuu mjini Brussels hazitasaidia kitu.Baada ya kipindi cha mwaka mzima cha utulivu wa kiuchumi, nchi nyingi za umoja wa ulaya zinaoenelea bora kufungamanisha bajeti zao na hali isiyokadirika.
Hata gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG lina maoni sawa na hayo.Linaandika:
"Usuhuba huu wa ghafla pamoja na kamisheni kuu ya Ulaya hautokani na hoja kwamba serikali kuu ya shirikisho inafikiria siku za mbele kupunguza matumizi.Hasha.Kinyume kabisa.Mpango wa kudhamini utulivu wa sarafu kama unavyopiogiwa upatu na kamisheni kuu ya umoja wa ulaya mjini Brussels unaonyesha kua dhihaka tuu.Kamishna anaeshughulikia masuala ya sarafu Joaquin ALMUNIA anavumilia hali hiyo sawa na anavyostahimilia ukuaji unaolega lega wa kiuchumi kutokana na sababu moja tuu:Hataki kusababisha mvutano mwengine pamoja na serikali kuu ya mjini Berlin.ALMUNIA anakihitaji kipindi hichi cha utulivu kwaajili ya sheria za sarafu ya Euro ambazo haziwezi kuakhirishwa."
Gazeti la LANDSHUTER ZEITUNG linahisi:
"Ni dhahiri,uamuzi wa kamisheni kuu ya umoja wa ulaya ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Berlin na Brussels.Wamesikilizana mapema tuu,shirikisho la jamhuri ya Ujerumani halitashitakiwa kwa kutofuata masharti ya kutuliza sarafu ya pamoja ikiwa kwa upande wake itakua tayari kuchangia vya kutosha katika makasha ya umoja wa ulaya.Lakini kama kuna ukweli ndani yake,hakuna ajuae.Dhahir ni kwamba Ujerumani na Ufaransa ndio madola yenye nguvu ndani ya umoja wa sarafu.Kamisheni kuu ya umoja wa Ulaya inaweza pengine kuvutana na Berlin au Paris lakini sio na wote wawili kwa wakati mmoja.Hapo kamiheni kuu haina hila.
Tukiingilia mada inayozusha mabishano humu nchini yaani mageuzi katika mfumo wa shirikisho,gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung linaandika:
"Jazba zilizowapanda viongozi wa serikali za majimbo katika awamu ya mwisho ya majadiliano,mara wakibishana wenyewe kwa wenyewe na baadhi ya wakati wakijitokeza na msimamo wa pamoja dhidi ya upande wa serikali kuu, kimsingi jazba hizo zimelengwa wateja wao nyumbani.Masharti makubwa makubwa yaliyotolewa dakika za mwisho mwisho na hasa na majimbo madogo ,yakifika hadi ya kutishia kutia munfda mageuzi ya mfumo wa shirikisho,hayastahili kupewa uzito mkubwa.Yanaonyesha tuu kinachojadiliwa ndanio ya kamisheni hiyo si cha kudharauliwa.
Ama kuhusu msimamo wa vyama ndugu vya Christian Democratic Union na Christian Social Union CDU/CSU kuhusiana na maombi ya Utururki ya kujiunga na umoja wa Ulaya ,gazeti la HAMBURGER MORGENPOST linaandika:
"Ni mbinu tuu ya kusaka mada ya kampeni ijayo ya uchaguzi baada ya kujikuta chapwa."Hakuna atakaesema wamekosea kwasababu demokrasia daima imekua ikipata nguvu kutokana na mabishano ya akisiasa.Kosa litajiri ikiwa wana CDU/CSU watajipigania bila ya kuwajali wengine."Ikiwa waturuki watajikuta wakilinganishwa na watu wanaotetea chuki,hawana lao isipokua kuowa wake au waume waliochaguliwa na wazee wao na kwamba kamwe hawawezi kuwa wazungu" basi watakaodhalilika ni mamilioni ya umma.Bila shaka mjadala lazma uwepo watui wajiulize kama Uturuki inapaswa kuwa mwanachama wa umoja wa Ulaya na kama kuna haja ya kuzidishwa juhudi za kujumuishwa katika jamii.Lakini muhimu ni juu ya namna mijadala hiyo inavyoendeshwa ili kuhifadhi masilahi ya kila upande.