yaliyoandikwa katika magazeti ya Ujerumani hii leo
19 Aprili 2005Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Manfred Kanther,kwa mshangao wa wengi amehukumiwa kutokana na kashfa ya fedha ilizojikusanyia chama cha CDU kinyume na sheria.Korti ya mjini Wiesebaden imekiuka madai ya mwanasheria mkuu,ilipomhukumu Manfred Kanther kifungo cha mwaka mmoja na miezi sita nje pamoja na kumtoza faini ya Euro 25 elfu.Wahariri wamagazetiya Ujerumani wameichambua kwa mapana na marefu mada hiyo,kama kwa mfano mhariri wa Berliner Kurier anaesema:
"Manfred Kanther ameistahiki hukumu hiyo.Aliamini,yeye na wasaidizi wake ndani ya chama cha CDU wangeweza kukiuka sheria na kuhamishia mamilioni ya fedha nchi za nje.Bwana yule yule,aliyekua akijinata na kujiangalia kama "mlinzi wa sheria na nidhamu",ndie aliyeziendeya kinyume sheria tena bila ya kupepesa.Kinachoniudhi zaidi mpaka sasa lakini ni ile hali kwamba kansela wa zamani Helmut Kohl bado hataki kusema chochote kuhusiana na mamilioni ya fedha aliyopokea kinyume na sheria.Nayeye pia,bwana Kohl anastahiki aonje makali ya sheria zetu.Akibidi basi alazimishwe."
Gazeti la mjini Düsseldorf la Handelsblatt limeandika:
"Ni shida kuamini kama hoja anazotoa Kanther zina ukweli ndani yake anapodai eti hajajitajirisha kutokana na fedha zilizokusanywa na chama cha CDU kinyume na sheria.Kanther mwenyewe alijitokeza kwa kiburi hapo mwanzo akijaribu kuhalalisha jinsi mamilioni hayo ya fedha yalivyofichwa na baadae kulazimika kutumiwa:Ni fedha na sio mikakati inayaoamua juu ya nguvu na ubora wa kampeni ya chama hiki au kile.Bila shaka Kanther amefaidika na mamilioni hayo.Katika serikali ya Helmut Kohl, Manfred Kanther alikua akisimamia sheria na nidhamu.Lakini amezivunja mwenyewe sheria na nidhamu hizo kwa kuziendeya kinyume kanuni zinazohusiana na vyama vya kisiasa na katiba pia.Ameihadaa nchi nzima, wapiga kura na marafiki zake chamani.Na hadidhi aliyoibuni pamoja na marafiki zake eti fedha hizo zimetokana na urithi wa wakfu wa wayahudi" ni ya aibu kupita kiasi."
Gazeti la Franakfurter Rundschau limeandika:
"Unataka kujua matokeo makubwa ya kisa hicho kwa chama cha CDU"? Angela Merkel.Koti la Helmut Kohl limeingia dowa,mlinzi wake wa zamani wa sheria na nidhamu kaponea chupu chupu kulala jela,chama cha CDU kimetozwa faini zisizokua na idadi na sheria zinazohusu vyama vya kisiasa zimebadilishwa.Yote sawa:Au si sawa.Muhimu na kitakachosalia nyoyoni mwa watu kwa muda mrefu zaidi ni chengine kabisa:Kwa kuporomoka vibaya kabisa, kansela wa milele amekitunukia bila ya kutaka chama chake,kile ambacho kwa khiari asingekifanya:nacho ni kuingia kizazi kipya madarakani.Chama cha CDU kimeingia kwa kasi katika utaratibu wa mageuzi kuliko chama chengine chochote kile humu nchini.Mkondo huu mpya umewezekana shukurani zimuendee mwenyekiti wake mpya bibi Angela Merkel.
Gazeti la OSTSEE-ZEITUNG la mjini Rostock limejishughulisha na kufungwa vituo vya jeshi la shirikisho Bundeswehr.Gazeti limeandika:
"Waziri wa megeuzi ya jeshi la shirikisho-Bundeswehr,Peter Struck hakuficha hata kidogo jana alipozungumzia kinaga ubaga juu ya kufungwa vituo vya jeshi.Hakuna hata kimoja kati ya vituo vilivyotajwa mwezi november uliopita kitakachosalimika na hatua hiyo.Na hata ikiwa serikali kuu itaamua katika kipindi cha miaka 5 ijayo kuvifunga vituo mia moja vyengine hakuna fedha zozote zitakazotolewa na viongozi wa mjini Berlin ili kufidia hasara hiyo au kuvitumia vituo hivyo vya kijeshi kwa mahitahji ya kiraia au kibiashara.Kinyume chake ndicho kitakachotokea.Hata vikiuzwa vituo hivyo vya kijeshi ambavyo baadhi vinabidi kusafishwa na vyengine kufanyiwa ukarabati,serikali kuu itataka pia kujikingia fedha.
Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung linachambua mkondo mpya unaofuatwa na chama cha walinzi wa mazingira Die Grüne kuhusiana na suala la kubuniwa aina mpya za silaha.
"Kwamba walinzi wa mazingira hivi sasa wanakubali shingo upande na kuunga mkono mtambo wa kinga ya angani Meads,mtu anaweza kuwaelewa.Kwasababu ,mojawapo ya faida chache zinazoweza kupatikana kutokana na mtambo huo ni kwamba mtambo huo ni mwepesi kuutumia kinyume na ule wa Patriot unaotumiwa hivi sasa na jeshi la shirikisho Bundeswehr.Waziri wa ulinzi anaeamini kua kutumwa wanajeshi wa Bundeswehr nchi za nje ni jambo la kawaida, anauangaliwa mtambo huo wa Meads ni wa maana.