Xi Jinping kukutana na Kim Jong Un mjini Beijing
4 Septemba 2025Matangazo
Rais wa China Xi Jinping na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un watakutana kwa mazungumzo mjini Beijing. Hayo yamesemwa leo na serikali ya mjini Beijing wakati kiongozi huyo wa Korea Kaskazini akifanya zaira ya nadra nchini China.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Guo Jiakun amesema viongozi hao wawili watafanya mazungumzo na kubadilishana mawazo kuhusu mahusiano kati ya China na Korea Kakszini na masuala ya masilahi ya pamoja.
Guo ameongeza kusema China iko tayari kushirikiana na Korea Kaskazini kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na mabadilishno ya uzoefu katika utawala.