SiasaAsia
Xi Jinping awasili nchini Kazakhstan
16 Juni 2025Matangazo
Rais wa China Xi Jinping amewasili leo nchini Kazakhstan kushiriki mkutano wa kilele kati ya China na mataifa ya kanda ya Asia ya Kati.
Kiongozi huyo wa China atafanya mikutano na viongozi wa Kazakhstan kabla ya kufunguliwa rasmi mkutano huo wa kilele kesho Jumanne.
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya kigeni ya China,mikutano hiyo itatowa ufafanuzi wa pamoja wa makubaliano ya ushirikiano wa baadaye.
Mkutano wa kilele ambao ni wa pili kufanyika kati ya China na mataifa ya Asia ya Kati, utawaleta pamoja Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, Rais Xi Jinping na viongozi wakuu wa nchi kutoka Uzbekistan, Tajikistan na Turkmenistan.