Xi ataka China na Umoja wa Ulaya washirikiane kupinga ushuru
11 Aprili 2025Matangazo
Rais wa China Xi Jinping ameuhimiza Umoja wa Ulaya kushirikiana na Beijing katika kupinga hatua za upande mmoja za uonevu na bughdha, akizungumzia ushuru uliowekwa na rais wa Marekani Donald Trump.
Shirika la habari la serikali ya China Xinhua limesema wakati alipokutana na waziri mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez leo Ijumaa mjini Beijing, rais Xi amesisitiza juu ya umuhimu wa ushirikiano kati ya umoja huo na China katika kupoza makali ya vita vya kibiashara vinavyoongezeka na Marekani.
Sanchez kwa upande wake amewaambia waandishi habari baada ya kukutana na rais Xi kwamba misuguano kuhusu biashara haitakiwi kukwamisha mashirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na China.