Xi aapa kuimarisha uhusiano wa kimkakati na Indonesia
13 Aprili 2025Rais Xi amesema hayo wakati wakipeana pongezi kwa kutimiza miaka 75 ya uhusiano wa kidiplomasia.
Shirika la habari la China Xinhua limeripoti kwamba Rais Xi alimwambia mwenzake wa Indonesia kwamba ushirikiano baina yao ni wa kimkakati na wenye athari kimataifa.
Beijing inajaribu kutanua ushawishi wake kwa mataifa mengine kuungana katika msimamo wa pamoja dhidi ya ushuru wa uagizaji bidhaa kutoka nje ya Marekani uliotangazwa na Rais Donald Trump.
Soma pia:China: Ushuru wa Marekani utasababisha madhara makubwa kwa nchi zinazoendelea
Xi atatembelea nchi nyingine za Kusini Mashariki mwa Asia zinazofungamana na Indonesia ikiwemo, Vietnam, Malaysia na Cambodia kuanzia Jumatatu, kwa lengo la kuimarisha uhusiano na majirani zake huku mvutano wa kibiashara na Marekani ukizidi kufukuta.