WTO latabiri kuporomoka kwa biashara ya dunia
17 Aprili 2025Shirika la biashara duniani,WTO limesema biashara ya bidhaa ulimwenguni, inatarajiwa kushuka kati ya asilimia 0.2 na 1.5 mwaka huu.
Shirika hilo limesema utabiri huo utategemea namna ushuru uliowekwa na rais Donald Trump utakavyosababisha athari.
Soma pia: China: Ushuru wa Marekani utasababisha madhara makubwa kwa nchi zinazoendeleaWTO imetahadharisha kwamba hali ya wasiwasi kuelekea sera ya biashara inaweza kusababisha athari mbaya kwa biashara duniani na kwamba tayari hivi sasa inaonesha biashara ya bidhaa duniani inatazamiwa kuporomoka kwa asilimia 0.2 katika mwaka huu.Soma pia:Trump atangaza ushuru mpya wa magari yanayoagizwa kutoka nje
Shirika hilo la biashara duniani limesema ushuru uliotangazwa na Marekani unaweza kuzidisha hali hiyo kuwa mbaya zaidi na biashara kushuka hadi kwa asilimia 1.5.