Thailand: Mgogoro wa kisiasa hautaathiri usalama wa mpakani
30 Agosti 2025Matangazo
Bangkok
Wizara ya Ulinzi ya Thailand imesema kukosekana kwa serikali rasmi nchini humo hakuaathiri usalama wa mipaka na Cambodia.
Taifa hilo linajaribu kujaza nafasi ya Waziri Mkuu iliyowachwa wazi baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kuondolewa kwa uamuzi wa mahakama ya Katiba.
Taifa hilo la kusini Mashariki mwa Asia, lilitumbukia katika msukosuko wa kisiasa siku ya Ijumaa, baada ya mahakama hiyo kumfuta kazi Waziri Mkuu Paetongtarn Shinawatra kufuatia namna aliyoshughulikia mzozo wa mpakani na Cambodia ikisema hakuzingatia kanuni za maadili.
Uamuzi huo umeiacha Thailandna kaimu Waziri Mkuu Phumtham Wechayachai, na Baraza la mawaziri la mpito litakalokuwepo hadi pale serikali mpya itakapoundwa mapema wiki ijayo.